TETESI ZA USAJILI LIGI KUU TANZANIA BARA TANGU KUMALIZIKA KWA LIGI HIYO MSIMU WA 2016/2017 - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Saturday, 3 June 2017

TETESI ZA USAJILI LIGI KUU TANZANIA BARA TANGU KUMALIZIKA KWA LIGI HIYO MSIMU WA 2016/2017SIMON MSUVA SAFARI IMEFIKA KUONDOKA YANGA

Timu tatu kutoka katika nchi tatu, sasa zinataka kumsajili winga mahiri wa Yanga, Simon Msuva. Timu hizo zinatokea katika nchi za Morocco, Misri na Afrika Kusini na Msuva amethibitisha hilo.

Kulingana na Saleh Jembe, Simon Msuva amedai kuwa ofa hizi ni kweli zimetua kwenye meza ya Yanga naye ana taarifa kamili kuhusu kila kinachoendelea.

AJIBU NA MKUDE RUKSA KUONDOKA SIMBA


Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema timu yake imechoshwa na kauli zisizoeleweka za wachezaji Jonas Mkude, Abdi Banda na Ibrahim Ajibu kuhusu usajili mpya, hivyo kamaa wanataka kuondoka ruksa, GLOBAL TV online iliripoti.

Mikataba ya wachezaji hao tayari imemalizika mwishoni mwa msimu uliopita na sasa wanatajwa kuondoka kwenda kwenye moja za klabu za hapa nchini.

DONALD NGOMA NA NIYONZIMA KUTUA SIMBA


Taarifa kutoka ndani ya Simba zimedai kuwa Donald Ngoma na Haruna Niyonzima wa Yanga wanakaribia kumwaga wino wa miaka miwili kutua Msimbazi, kwa mujibu wa Shaffihdauda .

Simba imekuwa ikiwawania Ngoma na Niyonzima tangu msimu uliopita ambapo sasa imeonekana kukaribia kuwanasa wote wawili kutokana na mikataba yao kufikia ukingoni. Ingawa italazimika kupunguza baadhi ya wachezaji wake wa kigeni kutimiza idadi ya wachezaji saba.

BATEZ NA OSCAR JOSHUA WA KUTIMKIA SINGIDA


Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya klabu hiyo, wachezaji hao wataondolewa Yanga na kupelekwa Singida inayofundishwa na Hans van Pluijm.

Kipa mkongwe wa Yanga Ally Mustafa na beki Oscar Joshua ni kati ya wachezaji watakaokuwepo kwenye kikosi cha Singida United katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, kama hawatakuwa katika kikosi hicho basi safari yao kwa upande wa Yanga itakuwa imeishia hapo.

KIPA WA LYON ANATAKA KUJIUNGA NA YANGA


Baada ya kumaliza mkataba wa kuichezea African Lyon kipa Mkameruni Youthe Rostand, amesema yupo tayari kujiunga na Yanga kwa ajili ya msimu ujao.

Rostand amesema kwa sasa ni mchezaji huru baada ya ligi kumalizika na Lyon kushuka daraja hivyo angependa kujiunga na timu kubwa inayoshiriki michuano ya kimataifa ambayo ni Yanga.

VIPI MCHAKATO WA HIMID MAO KWENDA DENMARK?


Kiungo mkabaji wa Azam FC, Himid Mao amesema mchakato wa majaribio aliokwenda kufanya Denmark ulienda vizur, anachosubiri sasa ni majibu ya mazungumzo baina ya pande mbili za klabu.

Mchezaji huyo amesema mkataba wake unaisha mwezi Novemba mwaka huu lakini ataangalia ofa yenye uzito zaidi kati ya Azam na klabu za nje ya nchi.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages