SATELLITE MICHEZONI - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Friday, 9 June 2017

SATELLITE MICHEZONI

 

   Poleni na majukumu wapenzi wasomaji Wa kipengele hiki.kwa Mara nyingine tena najitokeza kumulika mambo kadhaa yanayoendelea hususani kwa upande Wa mpira Wa miguu.


Juzi tar 7/6/2017 katika kipengele kama hiki cha satellite michezoni niliandika makala ambayo ilieleza jinsi gan tufanye / wapi tunakosea katika suala zima LA kuzifanya  club zetu zifanye vizur kimataifa . Mpaka sasa inawezekana watanzania bado tumeduwaa na kujiuliza inakuwaje club ya Everton inakuja kufanya tour Tanzania lakini inacheza na timu za Kenya?katika makala iliyopita niliandika kuwa je udhaifu Wa club zetu unasababishwa na ninia tunapokuwa kwenye mashindano kimataifa?


   Leo nirudi kushauri tena katika mfumo Wa usajili Wa timu za Tanzania, ili soka letu lisonge mbele basi ni vema tukawa na mfumo mzuri Wa jinsi ya kutafuta wachezaji,mfano wakati ligi inaendelea kuna kuwa na timu ya wataalamu  ambayo inatazama wachezaji wenye vipaj Wa ndani ya nchi ili hali nyingine ikiwa inajaribu  kutazama wachezaji kutoka nje ya nchi. kwa kufanya hivyo itasaidia sana  hata wakati ambapo ligi imesimama au imeisha kutohangaika tena na kuanza kugombania wachezaji ambao pengine kwa kuto tazama kwa makini tukaona wapo wachache kumbe wapo wengi wenye vipaji.


  pili ili timu zetu zifanye vizuri basi zifanye usajili kwa kufuata mahitaji ya mwalimu ili hata inapotokea kashindwa kufikia malengo basi ataondolewa kwa kuwa hatakuwa na kisingizio.kwa kuzingatia haya tunaweza tukapiga hatua mbele hata kama ikawa moja.mwalimu ndiye anayefahamu mifumo na nani anafaa kuingia kwenye mifumo yake ,kama tutakuwa tukiwapelkea wachezaji hawa walimu wetu ,kila siku tutaona timu zetu ni uchochoro pale tunapokuwa kwenye mashindano kama tunavyoona haya ya sports Pesa.Ni mategemeo yangu sasa kuona timu za Tanzania zinafanya vizuri kwenye mashindano.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages