SAMATTA APATA UZAMINI BENKI YA DTB - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Sunday, 18 June 2017

SAMATTA APATA UZAMINI BENKI YA DTBBenki ya Diamond Trust ‘DTB’ Jumapili ya Juni 18, imeingia mkataba wa miezi Sita na Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania na Timu ya KRC Genk ya Ubeligiji Mbwana Alli Samatta kuwa balozi wa Benki hiyo na kutumikia katika Nyanja tofauti.
Akizungumza mara baada ya kutambulishwa rasmi na Uongozi wa Benki hiyo Nahodha huyo wa Timu ya Taifa ya Tanzania, amesema kazi kubwa baada ya kuingia makubaliano ya kuwa Balozi wa benki hiyo ni kuendesha kliniki za kuibua Vibaji kwa vijana sehemu mbalimbali nchini.
-Mkataba ni wa muda wa miezi sita kuwa balozi wa DTB na kunashughuli nyingi ambazo nitazifanya ambazo zitahusisha pia michezo, kama Kliniki ambayo tumeifanya, kwa ajili ya kuhamasisha michezo” Alisema.

Samatta amesema amepokea makubaliano hayo na DTB kwa furaha kubwa na kuipongeza benki hiyo kwa mikakati tofauti kwa ajili ya kuboresha mchezo wa mpira wa miguu hapa nchi, ikiwemo kuidhamini ligi kuu soka Tanzania Bara.
-Sababu unaweza kusema Samatta ametumia kipaji chake na kufika alipo lakini kuna vipaji vingi ambavyo havijaibuliwa kwa hiyo kupitia DTB nafikiri vipaji vingi sana vitatoka na baadaye tunaweza kupata watu ambao wanauwezo sana” Alisema Samatta.
Samatta ambaye mara baada ya Kusaini mkataba huo aliendesha kliniki ya watoto zaidi ya 200 waliojitokeza katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam ameyaomba mashirika na makampuni mengine kujitokeza na kuiga mfano wa DTB ili kukuza soka la Tanzania.


Down load app hii moja kwa moja kwenye kifaa chochote cha Android ili kupata habari kutoka vyankende.com 👉👉http://www.androidcreator.com/apk/app204631.apk

No comments:

Post Bottom Ad

Pages