PRISON KUIFANYIA UMAFIA MAJIMAJI FC. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Friday, 23 June 2017

PRISON KUIFANYIA UMAFIA MAJIMAJI FC.


Wakati pilikapilika za usajili zikipamba moto, inaelezwa kuwa klabu ya Tanzania Prisons imepanga kuwasajili wachezaji wawili wa timu ya Majimaji ya Songea.

Taarifa kutoka mjini Mbeya zinasema wachezaji wanaonyatiwa na klabu hiyo ni Alex Kondo na Anton Matogolo.

Katibu Mkuu wa Prisons, Havintishi Abdallah alithibitisha klabu yake kuanza mawindo ya wachezaji mbalimbali kwa lengo la kuwasajili.

“Ni kweli tunaangalia huku na huko, na hao ni baadhi ya wachezaji tunaowahitaji kwenye timu yetu na hao ni baadhi yao. Ninachoweza kusema ni kuwa muda bado upon a wachezaji waliopendekezwa na mwalimu watasajiliwa,”alisema Havinitishi, aliyewahi kuwa nahodha wa kikosi hicho.

Aliongeza kuwa timu yake itaingia kambini mapema kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu na mashindano ya Kombe la Shirikisho (ASFC).

“Mwaka huu tumedhamiria kuanza maandalizi mapema na tunatarajia mwezi wa saba tuwe tumeanza maandalizi. Dhamira yetu ni kuhakikisha tunatoa ushindani mkubwa msimu unaokuja,”alisema.

Prisons ni miongoni mwa klabu chache ambazo bado hazijaanza usajili wa wachezaji watakaoitumikia msimu ujao. Klabu nyingine ambazo bado hazijafanya usajili wowote ni Mbao FC, Mtibwa Sugar, Ndanda, Ruvu Shooting na Majimaji.Download app hii moja kwa moja kwenye kifaa chochote cha Android ili kupata habari kutoka vyankende.com 👉👉http://www.androidcreator.com/apk/app204631.apk

No comments:

Post Bottom Ad

Pages