NYOTA WA TIMU YA TAIFA YA IVORY COAST AFARIKI DUNIA GAFRA AKIWA MAZOEZINI - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Monday, 5 June 2017

NYOTA WA TIMU YA TAIFA YA IVORY COAST AFARIKI DUNIA GAFRA AKIWA MAZOEZINI


Nyota wa timu ya Taifa ya Ivory coast na kiungo wa zamani wa Newcastle, Cheick Tiote amefariki dunia baada ya kuanguka ghafla akiwa mazoezini.

Tiote amepoteza maisha akiwa na umri wa miaka 30, alikuwa mazoezini katika kikosi cha Beijing Enterprises kinachoshiriki ligi daraja la pili.


Kiungo huyo raia wa Ivory Coast amejiunga na timu hiyo miezi mine tu iliyopita.

Alikimbizwa hospital zikiwa ni juhudi za kuokoa maisha yake lakini haikuwezekana.

Tiote amewahi kuwa kiungo tegemeo wa timu ya taifa ya Ivory Coast iliyokuwa inaongozwa na Didier Drogba.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages