NIYONZIMA SIMBA 100% MAMBO BAM,BAM.. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Monday, 19 June 2017

NIYONZIMA SIMBA 100% MAMBO BAM,BAM..


Kiungo wa kati wa klabu ya Yanga "Haruna Niyonzima" ameripotiwa kujiunga na watani wa jadi wa klabu hiyo ya mitaa ya Jangwani, Simba SC.

Niyonzima ambae hivi karibuni amekua gumzo katika mitandao mbalimbali na vyombo mbalimbali vya habari huku akihusishwa na tetesi za kuendelea kuitumikia klabu ya Yanga, usiku wa leo imeripotiwa kua Niyonzima amekubari ofa ya klabu ya Simba na kuingia mkataba wa miaka 2.


Mnyarwanda huyo ambae hivi karibuni alikua akiitumikia timu yake ya taifa katika mchezo wa maandalizi ya AFCON  imeripotiwa kupewa million 80 pamoja na kusomshewa watoto hii ni kwa mujibu wa chanzo kimoja kati ya vingi vilivyoripo.


Kwingineko chanzo kingine kineripoti kua niyonzima amepokea dau la Sh m100 na kukubari kujiunga na Msimbazi kwa kandarasi ya miaka miwili (2),huku  mmoja wa viongozi  kutoka Simba akithibitisha kujiunga kwa Niyonzima wakati rafiki wa karibu wa Niyonzima akigoma na kusema hajasaini bali alifanya nao mazungumzo.


Kwa haraka zaidi tunaweza kusema Niyonzama kwa simba 100%...
Huku wengine tukisema Niyonzima Simba mguu ndani mguu nje.


Down load app hii moja kwa moja kwenye kifaa chochote cha Android ili kupata habari kutoka vyankende.com 👉👉http://www.androidcreator.com/apk/app204631.apk

No comments:

Post Bottom Ad

Pages