Ni aibu morata kutua united - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Wednesday, 28 June 2017

Ni aibu morata kutua united


Meneja wa Hispania Vicente del Bosque amedai kuwa itakuwa ni "aibu" kumwona Alvaro Morata akihama Real Madrid kujiunga na Manchester United majira ya joto ikiwa dili litaafikiwa.
Inaaminika kuwa Mashetani Wekundu wanakaribia kukamilisha usajili wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye Jose Mourinho amemfanya kuwa shabaha yake kuu baada ya kushindwa kumpata Antoine Griezmann.
Del Bosque amekiri kwamba atavunjika moyo kumwona mchezaji huyo akiachana na mabingwa wa Ulaya, lakini haitaathiri nafasi yake kwenye kikosi cha timu ya taifa kuelekea michuano ya Kombe la Dunia mwakani.
"Jambo ambalo naona ni jema kwake, ni kwamba anacheza, lakini nadhani anafanya vizuri sana Real Madrid," aliwaambia waandishi. "Ni aibu kama ataondoka.
"Lakini mara zote nimekuwa nikisema kwamba ni utajiri mkubwa katika soka letu kwani wachezaji wetu wamekuwa na uwezo wa kucheza ughaibuni, na wameweza kupata namba. Kwake haitakuwa tatizo kwenye timu ya taifa ya Hispania."
Morata ambaye amefunga mabao 20 katika mechi 42 msimu uliopita, inasemekana amekatisha fungate yake mapema ili aweze kujumuika na timu yake ya taifaDown load app hii moja kwa moja kwenye kifaa chochote cha Android ili kupata habari kutoka vyankende.com 👉👉http://www.androidcreator.com/apk/app204631.apk

No comments:

Post Bottom Ad

Pages