NGOMA AFUATA NYAYO ZA NIYONZIMA ,ATUA RASIMI SIMBA.. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Friday, 23 June 2017

NGOMA AFUATA NYAYO ZA NIYONZIMA ,ATUA RASIMI SIMBA..


Baada ya klabu ya Simba kumnyakua mshambuliaji kutoka klabu ya Yanga,Haruna Niyonzima,Hatimae wamefanikiwa kuinyakua na saini ya nyota mwingine kutoka katika klabu hiyo.

Mabingwa hao wa Kombe la FA, wamempa Niyonzima mkataba wa miaka miwili na watamtambulisha siku yoyote punde baada ya mkataba wake Yanga kumalizika Julai 21, na sasa wameweka nguvu kuwanasa wachezaji wengine wawili wa Yanga akiwemo straika matata, Donald Ngoma.

Habari ambazo hazina shaka yoyote ni kwamba vigogo wa Simba watamsainisha straika Emmanuel Okwi kesho Jumamosi baada ya tajiri wao, Mohammed Dewji, aliyekuwa ugenini kurejea nchini.

Lakini mpya zaidi ni kwamba Simba wametua mezani kwa Ngoma na habari ambazo hazina shaka yoyote ni kwamba straika huyo yuko kwenye hatua nzuri ya mazungumzo na Mnyama.

“Yanga walikuwa wanahangaika tu kutaka kumpa mkataba mpya Niyonzima. Lakini alishindwa kuwaambia ukweli kwamba tulikuwa tumeshamalizana naye muda mrefu na muda ukifika tutamtambulisha kwani makataba wake unaisha mwezi ujao,” alisema kiongozi mwenye ushawishi mkubwa kwenye usajili wa Simba.

Kiongozi huyo aliiambia Mwanaspoti kwamba wako kwenye hatua nzuri ya mazungumzo na Ngoma raia wa Zimbabwe ambaye wanaamini kwamba kinachomtoa Yanga ni kuzungushwa maslahi yake na kuwa wao Simba wana uhakika wa kumpa kila anachotaka kwa wakati.

Habari za kushtua zaidi kutoka kwenye Kamati ya Usajili ya Simba ni kuwa mbali na Ngoma, kuna jina jingine kubwa ambalo litang’oka Yanga na kutua Msimbazi na litashtua wengi kwani hawatatarajia.

Simba wamesisitiza kwamba wakishamnasa Ngoma watafanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi chao tayari kwa Kombe la Shirikisho Afrika.

Simba wamepania kuwa na wachezaji wakali wawili mpaka watatu kwenye kila nafasi kumpa kocha wigo mpana wa kuchagua wakati wa kupanga kikosi kwani wamesisitiza wanautaka ubingwa wa Bara msimu ujao.


Down load app hii moja kwa moja kwenye kifaa chochote cha Android ili kupata habari kutoka vyankende.com 👉👉http://www.androidcreator.com/apk/app204631.apk

No comments:

Post Bottom Ad

Pages