NDOANO YA SINGIDA UNITED KUMNASA BARTEZ WA YANGA. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Thursday, 15 June 2017

NDOANO YA SINGIDA UNITED KUMNASA BARTEZ WA YANGA.


Mazungumzo baina ya kipa wa Yanga, Ally Mustapha 'Bartez' na uongozi wa Singida United, yamefika pazuri na wakati wowote anaweza kumwaga wino wa kuitumikia timu hiyo.

Chanzo cha habari kutoka Singida United, kinaeleza kwamba ndoano yao ilikuwa kwa Aishi Manula wa Azam, lakini Simba, wakawapiga bao ndipo walipoona kipa pekee ambaye atawafaa ni Bartez.

"Uongozi wa Singida upo jijini Dar es Salaam, Mungu akipenda kesho Bartez anaweza akasaini kwani ni kipa ambaye atawapa uzoefu kina Said Lubawa,"alisema.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages