NDANDA FC KUSUKA KIKOSI CHAKE UPYA,USAILI WA WACHEZAJI NA AJIRA MPYA KUJULIKANA KESHO.. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Sunday, 18 June 2017

NDANDA FC KUSUKA KIKOSI CHAKE UPYA,USAILI WA WACHEZAJI NA AJIRA MPYA KUJULIKANA KESHO..Uongozi wa Timu hiyo umewaalika wachezaji ambao wana sifa za kucheza Ligi kuu kujitokeza kwa majaribio ya timu hiyo yatakayofanyika katika uwanja wa Nangwanda sijaona, Jumatatu Juni 19 saa 9.00 jioni, zoezi ambalo litaendeshwa na zaidi ya Makocha saba kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mtwara.
Akizungumza na mtandao huu Katibu Mkuu wa Ndanda Fc Selemani Kachele, amesema wametumia mfumo huo ili kupunguza gharama za kuwasajili wachezaji ghali ambao amekiri kwa wakati huu hawawezi kuwasajili kwa kuwa wanakabiliwa na hali ngumu ya kifedha.

Tumeamua kufanya hivi ili kukwepa gharama kubwa za kusajili wa wachezaji ambao watakuwa wanahitaji pesa nyingi tunasajili lakini wachezaji wachache ili usitoke kama ilivyokuwa msimu uliopita," ameongeza Kachele. 
Katibu huyo amewataka vijana wengi kujitokeza katika zoezi hilo ili litakalosimamiwa na timu Viongozi wa Ndanda ili kuhakikisha wanapata wachezaji walio na kiwango kizuri ili kuisaidia timu hiyo msimu ujao. 
Kachele amesema kuwa klabu hiyo haitagharamia wachezaji hao na kuwataka kujipanga kwa gharama zote ikiwemo sehemu ya kulala yaani malazi, chakula na nauli.
-Wachezaji ambao watakuja kufanya majaribio wanatakiwa kujigharamia malazi, kula na kulala mpaka hapo majaribio hayo yatakapomalizika ila kwa wale ambao watachaguliwa na jopo la viongozi hao gharama zitakuwa chini ya timu," amesema Kachele. 

Msimu uliopita Ndanda walijipata katika hali ngumu ya kiuchumi pamoja na kupoteza wachezaji wengi waliokuwa na uzoevu.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages