MWNYI HAJI KUONDOKA JANGWANI, HII HAPA TIMU ANAKOELEKEA. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Wednesday, 7 June 2017

MWNYI HAJI KUONDOKA JANGWANI, HII HAPA TIMU ANAKOELEKEA.

Beki wa klabu ya Yanga, Mwingi Haji, jana aliweka wazi juu ya tetesi za yeye kusajiliwa na Simba kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Haji amesema kwamba, amekuwa akisumbuliwa na viongozi ili kupata saini yake, lakini bado alikuwa hajafanya maamuzi sahihi, lakini kwa sasa upo uwezekano mkubwa ya yeye kuelekea Mtaa wa Msimbazi.

Haji amekiri kwamba, mkataba wake na Yanga umekwisha na sasa yupo huru, ingawa bado anaipa nafasi kubwa timu yake ya zamani katika kupata saini yake, lakini bado hakuwa ameambiwa lolote.

“Viongozi wa Simba wamekuwa wakinisumbua wakitaka kunisajili katika kikosi chao, ila bado naipa nafasi kubwa timu yangu kwanza, japo mpaka sasa hawajanipa jibu lolote zaidi ya kuniambia nisubiri.

“Leo jioni (jana) ndio tutakaa kwa mara ya mwisho na baba yangu kulizungumzia hilo suala na kulitolea uamuzi, japo katika mazungumzo ya awali ameonyesha hana kinyongo na mimi kujiunga na Simba, si unajua sisi maisha yetu ni mpira, hatujasoma na nina familia inayonitegemea,” alisema Mwinyi.

Simba wanahitaji saini ya mchezaji huyo kwa ajili ya kusaidiana na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, ambaye nafasi yake imeonekana kutokuwa na msaidizi kwa muda mrefu, jambo ambalo linaweza kuigharimu timu kama ikitokea mchezaji huyo akipata tatizo lolote.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages