MTIBWA SUGAR YAPANDISHA MAKINDA WATANO KUTOKA TIMU B - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Sunday, 18 June 2017

MTIBWA SUGAR YAPANDISHA MAKINDA WATANO KUTOKA TIMU B


Wakata Miwa Kutoka Manungu Turiani Mkoani Morogoro,  Klabu ya Soka ya Mtibwa Sugar imefikia maamuzi ya kuwapandisha wachezaji wake watano kutoka timu B, ambao watakisaidia kikosi hicho katika msimu ujao wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara.
Msemaji wa Klabu hiyo, Thobias Kifaru Ligalambwike, ameuambia Mtandao Huu kuwa wamefanya maamuzi hayo makubwa kwa Mustakabali mzima wa Mtibwa Sugar na kwamba wameridhishwa na Viwango na wanaaimani kubwa kuwa wataleta ushindani katika ligi msimu ujao.
“Ni kweli tumewasajili wachezaji watano kutoka timu B, kwa kuwa wana uwezo mkubwa na tunaamini watakabiliana na ushindani kwenye ligi, tumeshauriana na Kocha Zubeiry Katwila na yeye kwa Moyo Mmoja amekubaliana na sisi kufanya hichi, naweza kusema tumepata baraka zake” alisema Kifaru.
Ligi ya Vijana.
Ikumbukwe katika ligi ya Vijana ilifanyika msimu uliopita Vijana wa Mtibwa Sugar walikuwa Tishio kwani mbali na Kushika nafasi ya Tatu, lakini pia walitolewa kwa Mbinde na Azam FC katika hatua ya Nusu Fainali.
Aidha Katika Michuano ya Ligi Kuu soka Tanzania Bara msimu wa 2016/17 Mtibwa ilimalizi Tanzania Bara katika nafasi ya nane kati ya timu 16 zilizokuwa zinashiriki ligi hiyo hivyo kuwaamini Vijana hao ni kuonesha namna gani Mtibwa Sugar wamekuwa wakiamini katika Soka la Vijana.Down load app hii moja kwa moja kwenye kifaa chochote cha Android ili kupata habari kutoka vyankende.com 👉👉http://www.androidcreator.com/apk/app204631.apk

No comments:

Post Bottom Ad

Pages