MKUDE,AJIBU SITI NXITO JANGWANI.. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Saturday, 10 June 2017

MKUDE,AJIBU SITI NXITO JANGWANI..


PAMOJA na ukimya mwingi wa klabu ya Yanga, lakini wakati wowote wanaweza kufanya maajabu kwa kuwanasa Ibrahim Ajib na Jonas Mkude, baada ya kufahamika kuwa ‘wanawanyatianyatia’ kimyakimya wachezaji hao wa Simba.

Yanga wamekuwa wakisaka wachezaji hao kwa muda mrefu sasa lakini ukimya wao ulioanza kuwatisha mashabiki wa klabu hiyo ya Jangwani, unakaribia kumalizwa kwa kishindo baada ya kigogo mmoja  kuwahakikishia saini za Ajib na Mkude.

Nyota hao wamekwishamaliza mkataba na klabu hiyo ya Msimbazi na hakuna taarifa za kuongeza mkataba mpya, hivyo Yanga washindwe wenyewe kumalizana nao.

Kigogo huyo mwenye ushawishi mkubwa Yanga ameliambia BINGWA jana kwamba, amewakataza wachezaji hao wasiongeze mikataba mipya Simba kwani atamalizana nao wakati wowote.

Pamoja na kuwapo kwa tetesi zinazomhusisha Ajib na kufukuziwa na klabu ya Singida United, lakini kigogo huyo amejitamba kuifunika klabu hiyo iliyopanda daraja msimu huu.

Kauli ya kigogo huyo imeanza kuhusishwa na taarifa za wachezaji hao kugoma kuongeza mikataba mipya na Simba, licha ya viongozi wao kuwabembeleza mchana na usiku ili kuwasainisha.

Kwa muda mrefu Mkude aligoma kuongeza mkataba mpya Simba, ambao waliamua kumsajili James Kotei ili kuziba pengo la kiungo mkabaji ambaye alikuwa akihusishwa na mpango wa kwenda kucheza soka Afrika Kusini, ila Yanga wanataka saini yake kwa udi na uvumba.

Kwa upande wake, Ajib hali ile ile kama kwa Mkude, naye pia amehusishwa na mpango wa kwenda Afrika Kusini ambako alishafanya majaribio msimu uliopita na sasa jina lake lipo kwenye orodha ya wachezaji wanaotakiwa na Yanga.

Hii ni mara ya pili kwa Mkude kuingia kwenye rada za Yanga, ambapo msimu wa 2015/16 klabu hiyo ya Jangwani ilikaribia kumsajili mchezaji huyo kwa dau la Sh milioni 80 lakini mwenyewe akagoma kusaini.

Yanga wanataka saini ya Mkude kuziba nafasi ya kiungo wa Zambia, Justin Zulu aliyeshindwa kuonyesha kiwango kizuri, huku wakimwinda Ajib kumrithi Donald Ngoma ambaye anataka kuondoka Yanga.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages