MKUDE NI MALI YA SIMBA - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Friday, 16 June 2017

MKUDE NI MALI YA SIMBA


Pamoja na tetesi kibao kuhusu mustakabali wake, kuna uwezekano mkubwa nahodha na kiungo mahiri wa Simba Jonas Mkude atabaki Msimbazi msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye chanzo cha kuaminika cha klabu hiyo Mkude anatarajia kuongeza mkataba na Simba ndani ya siku mbili wiki hii.

Mkude ataongeza mkataba baada ya mazungumzo na viongozi wake kukamilika na imeelezwa kila kitu kinakwenda sawa sawia.

Kwa mujibu wa SalehJembe , Mmoja wa viongozi amesema: “Sisi na Mkude, tuko vizuri na huenda akasaini ndani ya siku mbili.”

Jonas Mkude naye alipofuatwa alisema yuko katika mazungumzo na klabu hiyo na mazungumzo hayo yamefikia pazuri.

“Tusubiri kwanza ili kujua tumefikia wapi. Lakini mimi na viongozi tunajua tumefikia wapi,” alisema.

Tayari Ibrahim Ajibu ameamua kujiunga Yanga huku kukiwa na taarifa Abdi Banda na Mkude nao wamekuwa wakiwaniwa na watani wao wa jadi Jangwani.

“Suala la kuondoka nalijua mimi. Lakini sasa bado niko Simba na ninaendelea na mazungumzo, tuliachie hapo kwanza,” alisisitiza Mkude.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages