MKATABA WA MBARAKA YUSUPH WAZUA HAYA. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Tuesday, 20 June 2017

MKATABA WA MBARAKA YUSUPH WAZUA HAYA.Shirikisho la kandanda nchini TFF leo limetoa ufafanuzi juu ya usajili wa aliekua Mshambuliaji wa Kagera Sugar, Mbaraka Yusuph kuelekea Azam,hii ni baada ya malalamiko kutoka katika klabu ya Azamu ikilalamikia moja ya nakala ya mikataba ambayo mmoja unasema kua Mbaraka alisaini kagera sugar kwa mwaka mmoja huku nakala ya pili ikieleza kua mbaraka alisaini kwa miaka miwili.


Kwa mujibu wa Shirikisho hilo likijibu tuhuma hizo kupitia kwa msemaji imeelezwa kua "Ndugu zangu kuna mjadala unaendelea, kwenye baadhi ya magroup kuhusu mikataba miwili ya Mchezaji Mbaraka Yussuf Abeid. Ningependa ifahamike kwamba katika mfumo wa usajili kwa njia mtandao yaani TMS (Transfer Matching System),  taarifa huwekwa na meneja wa TMS wa klabu na wala siyo TFF. TFF wanaweza kusoma taarifa, lakini hawawezi kubadilisha. Kwa hiyo kama mchezaji aliomba nakala ya mkataba kilichotoka kwenye system ni halali mpaka ikithibitika kwamba taarifa zilizowekwa si za kweli. Na mkataba bila shaka ni kati ya mchezaji na klabu yake hivyo klabu inayochumbia haiwezi ku- conclude uhalali au kutokuwa halali kwa mkataba."Alfred Lucas

Imetolewa na..
Alfred Lucas
TFF MCO.


Down load app hii moja kwa moja kwenye kifaa chochote cha Android ili kupata habari kutoka vyankende.com 👉👉http://www.androidcreator.com/apk/app204631.apk

No comments:

Post Bottom Ad

Pages