MBARAKA YUSUPH ANUKIA MSIMBAZI .. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Sunday, 4 June 2017

MBARAKA YUSUPH ANUKIA MSIMBAZI ..


Makamu wa Rais wa klabu ya Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu’, amesema wamejipanga kuhakikisha wanamrudisha kundini mshambuliaji wa Kagera Sugar Mbaraka Yusuph.
 
Kaburu ameiambia Goal, kocha wao Joseph Omog ameridhia kiwango cha mshambuliaji huyo na angependa kufanya naye kazi kwenye kikosi chake cha msimu ujao.
 
“Kocha amesema anamuhitaji baada ya kumuona uwezo wake na sisi tumejipanga kuhakikisha tunamrudisha kundini ili kutimiza kile anachohitaji kocha wetu,” amesema Kaburu.
 
Kiongozi huyo amesema wameamua kuacha malumbano yaliyopo juu ya mkataba wa mchezaji huyo waliyekuwa wakimmiliki na sasa wanataka kuanza upya taratibu za kumsajili ili aweze kuitumikia timu yao msimu ujao.
 
Amesema anajua kwamba mchezaji mwenyewe anamapenzi makubwa na Simba, hivyo kazi yao haitakuwa ngumu kuipata saini yake.
 
“Nimchezaji wetu tulimkuza wenyewe kabla ya utata uliotokea msimu uliopita, lakini kwasababu Simba ni timu kubwa na tunahitaji huduma yake tumejiandaa kuhakikisha tunamrudisha ili kufaidi matunda yake,”amesema Kaburu.
 
Mbaraka Yusufu alikuwa moto wa kuotea mbali katika upachikaji wa mabao, akiwa na timu ya Kagera Sugar  na amemaliza msimu akiwa mfungaji bora namba tatu kwa kufunga mabao 12 huku akizifunga timu zote kubwa za Simba na Yanga.
 
Katika hatua nyingine Kaburu amesema timu yao imejiandaa vyema kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye mashindano ya Sport Pesa, yanayoanza kesho Jumatatu Jijini Dar es Salaam.
 
Kaburu amesema kila kitu kimekamilika na wana matumaini makubwa ya kuibuka na ubingwa huo kutokana na uimara wa kikosi walichokuwa nacho hivisasa.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages