MATUMAINI YA CHAMEROON KOMBE LA MABARA YADIDIMIA. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Friday, 23 June 2017

MATUMAINI YA CHAMEROON KOMBE LA MABARA YADIDIMIA.


Matumaini ya timu ya taifa ya Cameroon kufuzu katika hatua ya robo fainali kuwania kombe la dunia la mabara imedidimia, baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Australia katika mchuano wake wa pili Alhamisi usiku.

Simba wa Nyika, walianza vema mchuano huo kwa kupata bao la ufunguzi katika kipindi cha kwanza kupitia mshambuliaji wake Andre-Frank Zambo Anguissa.

Hata hivyo, nahodha wa Australia Mark Milligan aliisawazishia nchi yake katika dakika ya 60 ya mchuano huo.

Sare hii inaifanya Cameroon kuwa kibarua kigumu sana kufuzu katika hatua hii, inahitaji kuishinda Ujerumani na kuomba kuwa Chile inaishinda Australia.

Kundi la B, Chile wanaongoza kwa alama 4 sawa na Ujerumani huku Australia na Cameroon.

 Mechi za kutamatisha hatua ya makundi zitachezwa mwishoni mwa juma hili.

Jumamosi Juni 24 2017

Mexico vs UrusiNew Zealand vs Ureno

Jumapili Juni 25 2017

Ujerumani vs CameroonChile vs Australia

Down load app hii moja kwa moja kwenye kifaa chochote cha Android ili kupata habari kutoka vyankende.com 👉👉http://www.androidcreator.com/apk/app204631.apk

No comments:

Post Bottom Ad

Pages