Matic mulango wa kutokea huoo - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Saturday, 24 June 2017

Matic mulango wa kutokea huoo


Chelsea inakaribia kumsajili Bakayoko kutoka Monaco jambo ambalo litaacha mlango wazi kwa Nemanja Matic kuondoka darajani.
Tangu kuondoka kwa Jose Mourinho kiungo Nemanja Matic amekuwa haaminiwi na kocha wa sasa wa Chelsea Antonio Conte na hajapewa nafasi ya kutosha kushuka dimbani.
Lakini Mourinho bado anamuhitaji Nemanja Matic ili acheze na Paul Pogba katika kiungo cha Manchester United usajili ambao unasemwa kila siku katika vyombo vya habari na sasa umekaribia kutimia.


Taarifa zinasema Manchester United na kiungo huyo tayari wameshafikia makubaliano binafsi na sasa kinachosubiriwa ni kwa Chelsea kupokea ofa kutoka kwa United.
Mawasiliano kati ya kocha Jose Mourinho na kiungo huyo wa Serbia yanaonekana ni mazuri bado na wapo karibu, hii inaweza kuwa nafasi kwa Mourinho mwenyewe kufanya ushawishi wa kumnunua Matic.
Matic anahitajika United kwenda kushirikiana na Paul Pogba anayeonekana kuelemewa na majukumu mengi katikati ya uwanja huku msaidizi wake bora ambae ni Michael Carrick umri ukielekea ukingoni.


Down load app hii moja kwa moja kwenye kifaa chochote cha Android ili kupata habari kutoka vyankende.com 👉👉http://www.androidcreator.com/apk/app204631.apk

No comments:

Post Bottom Ad

Pages