Maneno ya kocha Bilali kwa kikosi cha Mbao. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Friday, 30 June 2017

Maneno ya kocha Bilali kwa kikosi cha Mbao.Kocha Athumani Bilali ameitaka Mbao FC kuacha kuwapa wachezaji wake mikataba mifupi inayoshindwa kuwa na faida kwao.

Mbao imepoteza wachezaji wake wanne wa kikosi cha kwanza waliochukuliwa na timu nyingine bure kutokana na kumalizika kwa mikataba yao.

Wachezaji waliondoka klabuni hapo ni kipa Benedict Haule, Salmin Hoza waliosajiliwa na Azam huku Pius Buswita akijiunga Yanga na Jamal Mwambeleko (Simba).

Kocha Bilali anayeinoa Stand United alisema Mbao inatakiwa kuachana na mfumo wa kuwapa mikataba ya mwaka mmoja wachezaji wake badala yake ifanye angalau miwili.

Alisema ndio maana Mbao FC imeambulia patupu kwa wachezaji wake wanne wamesajiliwa na Yanga, Simba na Azam.

“Siku hizi timu nyingi zimekuwa zikitoa mikataba ya kuanzia miaka miwili  na kuendelea hivyo na hii inafanya klabu iweze kupata fedha iwapo mchezaji akisajiliwa pengine”alisema Bilali.

Bilali alisema benchi la ufundi la timu hiyo liko vizuri katika kuibua vipaji na ndio maana wachezaji wake wamesajiliwa kwenye timu kubwa.

“Mbao ni wazuri kwa kutengeneza vipaji vya wachezaji wake ndio maana umeona Simba, Yanga na Azam zimewanyakuwa,” alisema kocha huyo.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages