MANCHESTER UNITED YAACHANA NA GREIZMANN YAMFUKUZIA NYOTA HUYU KUTOKA UJERUMANI. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Wednesday, 7 June 2017

MANCHESTER UNITED YAACHANA NA GREIZMANN YAMFUKUZIA NYOTA HUYU KUTOKA UJERUMANI.


KWANZA ilimtaka sana Antoine Griezmann wa Atletico Madrid, lakini baada ya straika huyo kudengua akidai atabaki hapo, klabu ya Man United sasa imeamua kuhamisha nguvu zao kwa mshambuliaji wa Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang.
United imepania kweli kumnasa hasa baada ya kusikia klabu ya PSG nayo inamuwania straika huyo mwenye thamani ya euro milioni 70.
Mtandao wa Daily Mirror umesema kuwa, straika huyo ni mchezaji anayeangaliwa kwa jicho kali na Kocha wa United, Jose Mourinho.
Inaeleweka kuwa, kwa sasa United ‘imepotezea’ dili la kumsajili Griezmann, baada ya Mfaransa huyo kudai kuwa anataka kubaki Atletico kufuatia uamuzi wa Mahakama ya Michezo (CAS) kutupilia mbali rufaa yao ya kupinga adhabu ya mwaka mmoja wa kutosajili.
Ripoti zilizopo nchini Ufaransa zinadai kuwa, klabu ya PSG imetoa ofa ya pauni milioni 61 kwa Aubameyang, lakini bado haijakubaliana na mchezaji.
Kutokana na hilo, United sasa haitapata shida kumsogelea straika huyo anayeonesha nia ya kuikacha Dortmund.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari za michezo wa Italia, Emanuele Giulianelli, Mourinho ‘ameshamvutia waya’ Aubameyang na kumuahidi mkataba wa miaka mitano.
Ni wazi Mourinho anatakiwa kumnyakua fasta Aubameyang, kwani atajikuta ana washambuliaji wawili tu kwenye majira haya ya kiangazi (Marcus Rashford na Anthony Martial).
Kama hiyo haitoshi, nahodha Wayne Rooney haeleweki na straika majeruhi Zlatan Ibrahimovic anatarajiwa kuondoka Old Trafford bure miezi michache ijayo.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages