MAJIBU YA KLABU YA SIMBA KWA ABDI BANDA - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Monday, 5 June 2017

MAJIBU YA KLABU YA SIMBA KWA ABDI BANDA


Klabu ya Simba imesema kuwa hadi sasa hakuna mchezaji yeyote wa klabu hiyo anayemaliza mkataba ambaye haijafanya naye mazungumzo akiwemo beki wake Abdi Banda.
Beki huyo aliyesajiliwa Msimbazi akitokea Coastal Union ya Tanga miaka miwili iliyopita, tayari alikwishawaaga mashabiki wa Simba mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho Mei 28 mwaka huu, huku akieleza kuwa uongozi wa Simba haukumfuata kwa ajili ya mazungumzo mapya baada ya mkataba wake kumalizika.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Klabu ya Simba Zakaria, Hanspoppe amesema alichokisema Banda ni uongo kwa kuwa tayari uongozi ulikwishafanya naye mazungumzo na kufikia muafaka wa kuachana naye.
“Alichokifanya Banda ni utoto, hakuna mchezaji anayemaliza mkataba wake ambaye hatujazungumza naye, kila mchezaji anafahamu akiwemo Banda, sasa nashangaa anatoka tena anazungumza tofauti,” Amesema Hanspoppe.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages