LUIZIO ATOA NENO USAJILI SIMBA SC. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Wednesday, 14 June 2017

LUIZIO ATOA NENO USAJILI SIMBA SC.


Mshambuliaji wa klabu ya Simba Juma Luizio , amesifu usajili wa timu hiyo na kuonesha matumaini ya timu hiyo katika mashindano ya kimataifa.
Luizio amesema“Simba usajili wanaoufanya mpaka hivi sasa wanaonyesha kabisa kuwa hawaendi kushiriki bali wanaenda kushindana kutokana na kuwa wamesajili wachezaji wazoefu ambao sio wageni kabisa wa mashindano ya kimataifa,” .
Luizio pia alisema kuwa kuja kwake kumemfanya aongezeke kujiamini kutokana na kupata mechi za mara kwa mara kucheza tofauti na ambavyo ilivyokuwa Zesco licha ya kuwa alikuwa akisumbuliwa na majeraha.
“Simba nimepata nafasi nyingi za kucheza, nimeongezeka kujiamini na nina utimamu wa mwili, baada ya kucheza hapa tofauti na ilivyokuwa Zesco kwa hiyo kwa hali hii naweza nikacheza sehemu yoyote ile hata ikiwa sio Simba,” alisema.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages