KLABU YA YANGA YATHIBITISHA KUMUACHA NIYONZIMA - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Wednesday, 21 June 2017

KLABU YA YANGA YATHIBITISHA KUMUACHA NIYONZIMAKlabu ya Yanga SC kupitia kwa Katibu Mkuu Boniface Mkwasa imethibitisha kushindwa kumudu dau la kuinasa saini ya Mshambuliji mnyarwanda Haruna Niyonzima.


Yanga kupitia ukarasa wake wa facebook imeandika juu ya kushindwa kwa klabu hiyo kufikia makubariano  naye.

Katika taarifa hiyo yanga imeripoti:- "Taarifa kwa Umma,Klabu ya Yanga kupitia kwa katibu mkuu Charles Boniphace Mkwasa, inapenda kuwajulisha wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga juu Mchezaji raia wa Rwanda Haruna Niyonzima ambaye amekua Mchezaji wetu kwa misimu 6 mfululizo katika kiwango cha juu.
Hata hivyo Haruna Niyonzima bado ana mkataba mpaka mwezi Julai na Yanga Sc, lakini hatutaweza kuendelea kuwa nae kwa msimu ujao kwani hatukuweza kufikia mwafaka katika mazungumzo yetu na yeye licha ya timu yetu kuwa na nia za kuendelea nae kwa misimu miwili ijayo.
Klabu inamtakia kila la kheri katika maisha yake na soka kwa ujumla.

Hata hivyo Niyonzima amekua akihusishwa na tetesi za kujiunga na wapinzani wa klabu hiyo Simba SC .


Down load app hii moja kwa moja kwenye kifaa chochote cha Android ili kupata habari kutoka vyankende.com 👉👉http://www.androidcreator.com/apk/app204631.apk

No comments:

Post Bottom Ad

Pages