MADRID YAANDIKA REKODI MPYA KATIKA FAINALI YA AINA YAKE - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Saturday, 3 June 2017

MADRID YAANDIKA REKODI MPYA KATIKA FAINALI YA AINA YAKE


Klabu ya Real Madrid imefanikiwa kuweka rekodi baada ya kuutwaa ubingwa wa Ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya kuinyuka klabu ya Juventus kipigo cha paka katika mchezo uliopigwa katika mji wa Cardif.

Katika mchezo ulioanza kwa timu zote kucheza kwa tahadhari kubwa huku kila mmoja akimchunga mwenzake umeshuhudia nyota wa soka Duniani Christiano Ronaldo akipachika goli la kwanza mnamo dakika 20' na katika piga nikupige ya hapa na pale Juve wanarudisha goli mnamo dakika ya 27' magoli yaliyodumu hadi kumalizika kwa kipindi cha kwanza.

Kipindi chapili kilianza kwa timu zote kucheza kwa umakini kabla ya klabu ya Real madrid kumakinika zaidi na kutumia nafasi walizo zipata kwa kupachika magoli matatu, magoli yaliyotiwa kimiani na Casemiro huku goli la tatu likifungwa na mnyama Christiano Ronaldo kabla ya Marco Asensio kukamilisha kalamu ya magoli kwa kugongelea msumali wa mwisho na kufanya ubao wa magoli kusomeka 4-1.
Hata hivyo Madrid imetwaa ubingwa huo kwa mara ya pili mfululizo huku ikitwaa ubingwa huo kwa kuilaza timu ambayo zilikutana katika fainali kama hii mnamo mwaka 1997.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages