KIAMA JANGWANI,TAMBWE NAE HUYOO.. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Monday, 19 June 2017

KIAMA JANGWANI,TAMBWE NAE HUYOO..Mshambuliaji wa Yanga na timu ya taifa ya burundi, Amis Tambwe huenda msimu ujao akaichezea Majimaji, baada ya kocha wa timu hiyo Kally Ongala, kusema atamsajili endapo timu yake itashindwa kumpa mkataba mpya.


Kocha huyo amesema  anavutiwa na uwezo wa mshambuliaji huyo wa kimataifa kutoka Burundi na yupo tayari kumshawishi ahamie timu yake msimu ujao kama Yanga wataamua kuachana naye.
“Tambwe ni mchezaji mzuri na anauwezo mkubwa katika washambuliaji wanaocheza timu za Ligi Kuu, binafsi natamani kufanya naye kazi kwenye kikosi changu endapo timu yake itaamua kuachana naye,”amesema Ongala.
Kocha huyo aliyeinusuru Majimaji kushuka daraja kwa msimu wa pili mfululizo, alisema timu yake inakosa mshambuliaji mwenye uzoefu kama wa Tambwe, hivyo kumpata yeye itakuwa ni msaada tosha wa kuifanya timu hiyo msimu ujao kufanya vizuri kwenye ligi na kumaliza kwenye nafasi za juu.


Hata hivyo klabu ya Yanga mpaka sasa wamekuwa kimya kuhusiana na kumuongeza mkataba mpya mshambuliaji huyo ambaye msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, alimaliza nafasi ya tatu kwa kuifungia timu hiyo mabao 11.


Tambwe yupo huru, baada ya kumaliza mkataba wa kuwatumikia Mabingwa hao wa Tanzania Bara, kwa mafanikio makubwa katika kipindi cha misimu mitatu aliyoichezea.

Down load app hii moja kwa moja kwenye kifaa chochote cha Android ili kupata habari kutoka vyankende.com 👉👉http://www.androidcreator.com/apk/app204631.apk

No comments:

Post Bottom Ad

Pages