KAULI YA SADI KAWEMBA (AZAM) BAADA YA KUTENGULIWA KATIKA NAFASI YAKE. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Thursday, 1 June 2017

KAULI YA SADI KAWEMBA (AZAM) BAADA YA KUTENGULIWA KATIKA NAFASI YAKE.ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa klabu ya soka ya Azam FC, Saad Kawemba, amekubali yaishe baada ya kuondolewa kwenye nafasi hiyo iliyochukuliwa na mwanahari Abdul Mohamed.

Kawemba alijiunga na klabu hiyo ya Azam tangu mwaka 2014, akitokea katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) alikokuwa na nafasi ya Ukurugenzi wa Mashindano.

Hatua hiyo ya Azam kumpiga chini Kawemba imekuja baada ya bosi huyo aliyekuwa na mkataba wa miezi sita kumaliza mkataba, huku klabu hiyo ikipanga kutomuongezea mkataba mwingine.

Akizungumza na BINGWA jana, Kawemba alisema ni jambo la kawaida kwa kiongozi kuachia wadhifa wake na kutafuta sehemu nyingine ili kufanya mambo mengine.

“Suala la kuondoka ni jambo la kawaida, lakini kuna mambo bado tunaendelea kuzungumza na viongozi wa klabu hiyo kama tukishindwa kukubaliana ndio utakuwa mwisho wangu Azam,” alisema Kawemba.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages