KAPOMBE MANURA WATINGISHA SIMBA - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Tuesday, 6 June 2017

KAPOMBE MANURA WATINGISHA SIMBA


Hata hivyo, uwezekano wa Simba kuwasajili Kapombe na Manula bado unalegalega baada ya taarifa ya awali kutoka kwa uongozi wa Azam kuweka wazi kutokuwa tayari kuwaachia nyota hao.
Tangu kumalizika kwa msimu huu wa Ligi Kuu Bara, Simba ilitajwa kuwa mbioni kumalizana na nyota hao waliopo kwenye kikosi cha timu ya Taifa 'Taifa Stars'.


Akizungumza na gazeti hili jana, Ofisa Habari wa Azam, Jaffar Iddi, alisema uongozi wa klabu yake upo kwenye hatua za mwisho kuwasainisha mikataba mipya nyota hao.
"Niwatoe hofu mashabiki wa Azam, wachezaji hawa wakati wowote kuanzia sasa watasaini mikataba mipya na hakuna hata mmoja atakayeondoka," alisema Iddi.
Alisema maneno yanayosemwa kuwa nyota hao wanakaribia kujiunga na Simba hayana mantiki yoyote.Simba imepania kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa watakayoshiriki kwa mara ya kwanza baada ya miaka minne kupita, hivyo ipo kwenye mchakato wa kukiboresha kikosi chao na wanaona nyota hao wanaweza kuwasaidia kutokana na kuwa wazoefu wa mechi za kimataifa.


Benchi la ufundi la Simba chini ya Kocha wake Mcameroon Joseph Omog, linataka asajiliwe golikipa mwenye uwezo mkubwa ili kumpa changamoto kipa wa sasa Mghana Daniel Agyei na tayari viongozi wameona Manula anafaa kwa nafasi hiyo. 

No comments:

Post Bottom Ad

Pages