KAGERA SUGAR WAMNASA GOLIKIPA HUYU... - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Tuesday, 13 June 2017

KAGERA SUGAR WAMNASA GOLIKIPA HUYU...


KAGERA Sugar imemsajili kwa mkataba wa mwaka mmoja kipa Said Kipao kutoka kituo cha kuwanoa makipa kinachomilikiwa na Peter Manyika.

Manyika ni kipa wa zamani wa Yanga, Mtibwa Sugar na Taifa Stars.

Kabla ya kutua Kagera, Kipao aliichezea JKT Ruvu iliyoshuka daraja msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na BINGWA jana, Manyika alisema tayari amemalizana na  Kagera Sugar hivyo ni mali halali ya klabu hiyo.

“Tulifanya mchakato wa usajili wa mchezaji huyo kwa siri kubwa na kwamba, wameamua kumsajili baada ya kuona uwezo wake JKT Ruvu, bado makipa wapo na tunatoa fursa kwa timu za Ligi Kuu kusajili.

“Sina wasiwasi na makipa wanaotoka kwenye kituo changu, wana kiwango  kizuri kwa sababu  wanazingatia mazoezi  na mbinu wanazofundishwa na mwalimu,” alisema Manyika ambaye  mwanaye Manyika Junior anayeidakia Simba.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages