JORDAN PICKFORD KUTUA EVERTON. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Friday, 16 June 2017

JORDAN PICKFORD KUTUA EVERTON.


Everton imetangaza usajili wa mlinda mlango Jordan Pickford kwa ada ya rekodi katika klabu hiyo.

Pickford alikuwa miongoni mwa wachezaji wachache waliokuwa waking'ara Sunderland iliyoshushwa daraja kutoka Ligi Kuu Uingereza, na mara moja klabu zenye majina makubwa zimekuwa zikimwania.

Arsenal walikuwa wakipewa nafasi kubwa kuinasa saini yake, lakini Everton walikuwa na shida zaidi na kipa huyo wa Uingereza kikosi cha umri chini ya miaka 21 baada ya Maarten Stekelenburg na Joel Robles kushindwa kutumia vema fursa zao.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa sasa yupo kwenye majukumu ya kimataifa kwenye michuano ya Ulaya umri chini ya miaka 21, lakini amefanikiwa kufanya vipimo na kusaini mkataba wa miaka mitano.

Imeripotiwa kuwa Pickford atagharimu takribani paundi milioni 30, na paundi milioni 25 zimeshatangulizwa na nyingine zitalipwa.

Pickford anaondoka Stadium of Light akiwa amecheza mechi 35 katika michuano yote, pia akiwa amecheza kwa mkopo Preston North End na Bradford City.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages