HUU HAPA USAJILI ULIOKAMILIKA HADI SASA LIGI KUU TANZANIA ... - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Friday, 16 June 2017

HUU HAPA USAJILI ULIOKAMILIKA HADI SASA LIGI KUU TANZANIA ...



ALLY SHOMARI WA MTIBWA ATUA MSIMBAZI

Klabu ya Simba imefanikiwa kumsajili Ally Shomari na ametua rasmi Msimbazi kwa mujibu wa habari kutoka kwa klabu hiyo mashuhuri Ligi Kuu Bara.

Kiungo huyo kiraka kutoka klabu ya Mtibwa Sugar, ametambulishwa rasmi na makamu wa Rais wa Simba Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ kwa kukabidhiwa jezi ya klabu hiyo.



SHOMARI KAPOMBE ASAINI SIMBA MIAKA MIWILI

Wekundu wa Msimbazi wamemalizana na Shomari Kapombe katika maandalizi yao kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na mechi za Kimataifa.

Si hadithi kama ilivyokuwa awali, Kwani Jumapili Kapombe alisaini mkataba wa miaka miwili.

Mchezaji huyo mahiri amerudi nyumbani akitokea Azam FC aliyojiunga nayo baada ya kuacha soka la Ufaransa.



AISHI MANULA ASAINI MIAKA MIWILI SIMBA

Kipa wa Azam FC Aishi Manula, amemalizana na Simba kwa kusaini mkataba wa miaka miwili.

Taarifa zinaeleza, Simba wamemalizana na Manula mara tu baada ya kambi ya timu ya taifa iliyocheza jana dhidi ya Lesotho.

“Kweli amesaini miaka miwili, Simba inaendelea na kazi yake. Tafadhari waambieni wanachama na mashabiki watuamini, tunajitahidi kufanya kazi yetu,” kilieleza chanzo.

Tayari Simba ilikuwa imezungumza na Manula, lakini akaondoka kusafiri na timu ya taifa iliyoweka kambi nchini Misri. Manula anakuwa mchezaji wa pili baada ya John Bocco kumalizana mapemaa na Simba.



JOHN BOCCO ATUA SIMBA RASMI

Mshambuliaji John Raphael Bocco amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Simba, baada ya kumalizana na timu aliyoichezea kwa misimu 10 mfululizo Azam FC.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, ameiambia Goal, wameshamalizia na Bocco, na kwasasa ni mali yao hivyo msimu ujao ataonekana akiwa amevalia jezi nyekundu na nyeupe.

“Nikweli Bocco tumemalizana naye baada ya kumpa mkataba wa miaka miwili ni mchezaji mzuri ambaye hata kocha Joseph Omog ameridhishwa na usajili wake,” amesema Hans Poppe.



AZAM FC YAMSAJILI KIPA WA MBAO, BEN HAULE

Azam FC inamsajili kipa wa Mbao FC Benedict Haule baada ya aliyekuwa kipa wake wa kwanza kwa misimu mitatu iliyopita, Aishi Manula kusaini Simba SC.

Azam wamemrejesha kipa wao huyo wa zamani kwa mkataba wa miaka miwili.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages