HAYA SASA JUMA NYOSO AANZA MAKEKE YAKE HATA KABRA YA LIGI KUU KUANZA.. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Sunday, 18 June 2017

HAYA SASA JUMA NYOSO AANZA MAKEKE YAKE HATA KABRA YA LIGI KUU KUANZA..


Mapema wiki hii Kagera Sugar chini ya Kocha Mecky Maxime ilimsajili Nyosso akiwa ametoka kwenye adhabu ya kufungiwa miaka miwili kwa kosa la kumdhalilisha aliyekuwa nahodha na mshambuliaji wa Azam FC John Bocco na kipindi hicho Nyosso alikuwa akiichezea klabu ya Mbeya City

Nyosso ameanza msimu mpya kwa kusema machache ya moyoni huku akurusha kombora kwa waliodhania kua ndo mwisho wa safari yake katika soka huku akisema wajiandae atakapo kutana nao, hata hivyo amesema anafurahia kumaliza adhabu yake na sasa anarejea uwanjani akiwa amejifunza vitu vingi na hawezi kurudia kufanya vitendo vya udhalilishaji.

“Nimefurahi kujiunga na Kagera Sugar nimerudi kupiga kazi na hivyo sitazungumza kwa mdomo bali vitendo,hivyo mtu yeyote atakayetaka kuona uwezo wangu aje tukutane uwanjani”


Nyoso aliongeza kwa kusema “”Muda wote niliofungiwa adhabu ilikuwa ikiniumiza moyoni na sasa mimi ni mtu mpya na nilikuwa nafanya mazoezi ya nguvu ndiyo maana nasema sasa ni kupiga kazi tu””.


Aidha alisema “Namshukuru Mungu kwanza kwa kuniwezesha kumaliza adhabu hii lakini kama unavyojua mimi siku zote huwa siyo msemaji sana katika vyombo vya habari, mimi kazi tu”.

Down load app hii moja kwa moja kwenye kifaa chochote cha Android ili kupata habari kutoka vyankende.com
 http://www.androidcreator.com/apk/app204631.apk
BOFA HAPA

No comments:

Post Bottom Ad

Pages