Haondoki jangwani.. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Sunday, 25 June 2017

Haondoki jangwani..


Kiungo wa wakimataifa wa Zimbabwe Thabani Kamusoko, amewatoa hofu mashabiki wa Yanga kwa kusema atasaini na kuendelea kuichezea timu hiyo msimu ujao.


Kamusoko ameiambia Goal, japo amepokea ofa mbalimbali kutoka timu za Tanzania na nyumbani kwao Zimbabwe, lakini ameona ni vyema akabaki Yanga kwa sababu kile alichokusudia bado hajakitimiza.
“Mashabiki wa Yanga waondoe hofu juu yangu nitabaki hapa kwa sababu kitu nilichohitaji ambacho ni ubingwa wa Afrika au hata kucheza fainali bado sijapata na naamini msimu ujao tunaweza kufanya vizuri na kutimiza hilo,” amesema Kamusoko.
Kiungo huyo amesema anaimani kubwa na wachezaji wapya watakaosajiliwa na timu hiyo kuwa wataongeza nguvu na kufanya vizuri pale waliposhindwa hasa kwenye michuano ya kimataifa.


Kamusoko amesema anatambua kuwa msimu ujao utakuwa mgumu kwao kutokana na timu nyingi kujiandaa lakini watafanya maandalizi mazuri chini ya kocha wao George Lwandamina na kufanya vizuri ikiwepo kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Yanga kwa sasa ipo katika wakati mgumu kuhakikisha inawabakiza nyota wake waliomaliza mikataba, baada ya wapinzani wao Simba kuonekana kuwanyemelea na tayari imeshafanikiwa kumchukua kiungo wake wa kimataifa Haruna Niyonzima raia wa Rwanda.


Baada ya Haruna Niyonzima, kuachana na Yanga kufuatia mkataba wake kumalizika Kamusoko, amesema atabaki kwa sababu bado anamambo makubwa ya kuifanyia timu hiyo.Down load app hii moja kwa moja kwenye kifaa chochote cha Android ili kupata habari kutoka vyankende.com 👉👉http://www.androidcreator.com/apk/app204631.apk

No comments:

Post Bottom Ad

Pages