HAJI MANARA: " SHAFIH DAUDA ACHA KUFUGA MARADHI FUGA KUKU UPATE MAYAI NA KITOWEO" KAULI KALI YA MANARA KWA SHAFIH - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Thursday, 22 June 2017

HAJI MANARA: " SHAFIH DAUDA ACHA KUFUGA MARADHI FUGA KUKU UPATE MAYAI NA KITOWEO" KAULI KALI YA MANARA KWA SHAFIH


Alichoandika Haji Manara, afisa habari wa Simba aliesimamishwa na TFF kwenda kwa Shafih Dauda

SHAFIH DAUDA acha kufuga maradhi,fuga kuku upate mayai na kitoweo
______________________________________________

Na :Haji S Manara

Shafih Daud ni mmoja katika  watu wa soka hapa nchini,ni rafiki yangu tunaoongea muda mrefu hususan masuala ya mchezo huu murua,uliyobeba maisha yangu,pia ni kijana mwenzangu tunaoheshimiana sana,kiasi cha kwamba sijawahi kwa namna yoyote ile kukwazana nae,hata kama tunatofautiana kimtazamo katika baadhi ya mambo, hususan ya Soka.

Wengi mnakumbuka sakata la Ramadhan Singano jinsi lilivyo karibia kuvunja uhusiano wetu kwa jinsi alivyolivalia njuga bila kuujua ukweli,lakini mwishowe ni yeye juzi tu aliandika kuwa Singano anataka kuvunja mkataba wake ambao hadi sasa naamini si HALALI, mkataba ulioidhinishwa na TFF huku akiwa na mkataba na klabu nnayoisemea na kuishabikia Simba SC, lakini hayo yashapita, undugu na uhusiano wetu bado upo pale pale.
Hata jana baba yangu mdogo Kassim Manara, aliyepo nchini kwa likizo ya majira ya kiangazi toka aishipo huko Belgium, alitaka kuongea nae kupitia simu yangu,na waliongea mengi, huku akimsifu ni kijana mstaraabu ambae hajawahi kukosa kwenda kumsalimia pale aendapo kule Belgium ama Belige kama waitavyo Wacongo,kila apatapo nafasi ya kwenda huko, hakika huyu na Eddo Kumwembe ni washabiki wakubwa wa wazee wangu, Sunday na Kassim Manara, hata Eddo alimtembelea mwanasoka huyo mahiri wa zamani na wa kwanza nchini kutikisa nyavu za Santiago Barnabeu,wakati akicheza soka la kulipwa kule Austria.
Lakini leo nimeamua kumwambia ukweli *’swahiba’* wangu huyo, ukweli ambao ninaamini ataufanyia kazi kwa haraka,ili kulinda image yake na ya blog anayoiongoza na iliyo maarufu miongoni mwa blogs za michezo nchini.
Asubuhi nilimpigia kumweleza dukuduku langu, juu ya makala zinazoichafua klabu na uongozi wa Simba, zinazoandikwa na mtu aitwae *Mbolembole*, mtu huyu ni mgeni katika Soka, simjui,sina rekodi nae zozote, ama za uandishi wa michezo, au hata uchambuzi kama walivyo Shafih na kina Eddo.
Mtu huyu kila kukicha huandika vitu vibaya kuhusu Simba, hutuchokoza na kutaka kuaminisha watu Simba ni klabu ya hovyo na inaongozwa na watu wasiojua lolote kuhusu football.
Anaitumia blog ya Shafih kuidhalilisha klabu yetu.


Download app hii moja kwa moja kwenye kifaa chochote cha Android ili kupata habari kutoka vyankende.com 👉👉http://www.androidcreator.com/apk/app204631.apk

No comments:

Post Bottom Ad

Pages