HABARI ZOTE ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUNE 07 2017.. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Wednesday, 7 June 2017

HABARI ZOTE ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUNE 07 2017..


WENGER AZUNGUMZA NA LACAZETTE

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amefanya mazungumzo na Lyon kuhusu usajili wa mshambuliaji Alexandre Lacazette, kwa mujibu wa The Sun .

Kocha huyo Veterani alikuwa Ufaransa wiki hii na Ivan Gazidis kukutana na rais wa Lyon Jean-Michael Aulas, akiwa na tumaini la kukubaliwa kufanya biashara hiyo.

SOUTHAMPTON YAMTAKA TUCHEL

Southampton wanataka kumtupia virago meneja wao Claude Puel na kufanya mkataba na kocha wa zamani wa Borussia Dortmund Bw. Thomas Tuchel kama mbadala wake, kwa mujibu wa  The Sun .

Puel ataondolewa majukumu yake baada ya kuinoa klabu hiyo msimu mmoja, na Saints wanaamini wataweza kumshawishi Tuchel kutua St. Mary.

BOURNEMOUTH YAFANYA MAZUNGUMZO NA TERRY

Bournemouth wamekaribia kumsajili beki wa Chelsea John Terry bada ya mazungumzo na meneja Eddie Howe, kwa mujibu wa The Sun .

Nahodha huyo wa zamani wa Uingereza atakuwa akilipwa £100,000 kwa wiki.

UTD & CHELSEA ZAMTOLEA MACHO DYBALA

Manchester United na Chelsea zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala, kwa mujibu wa Mundo Deportivo .

United wana kila dalili ya kumkosa Griezmann baada ya rufaa ya Atletico Madrid kufungiwa usajili kushindwa, na wanaamini Dybala ni mbadala sahihi.

MAN UTD YATOA £113M KUMSAJILI MBAPPE

Manchester United wametoa dau la paundi milioni 113 kwa ajili ya kinda matata wa Monaco Kylian Mbappe, kwa mujibu wa  The Daily Mail .

Habari zinadai kuwa Manchester City na Real Madrid ni klabu zinazoiwania saini ya mchezaji huyo mahiri wa Ufaransa.

BAYERN WANAMTAKA LUKAKU

Bayern Munich wameonyesha nia ya kutaka kumsajili Lukaku ambaye yupo kwenye rada za Manchester United na Chelsea, Manchester Evening News  limesema.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji anatarajiwa kuondoka Everton majira ya joto baada ya kukataa kusaini mkataba mpya, na miamba wa Ligi ya Uingereza wanaifukuzia saini yake.

TORRES HISPANIA PAMSHINDA, AENDA MEXICO


Fernando Torres anakaribia kujiunga na klabu ya Mexico Queretaro, kwa mujibu wa  ESPN .

Nyota huyo wa Atletico Madrid yupo katika mazugumzo yaliyochangamka na klabu hiyo ya Liga MX na anaweza kujiunga na timu hiyo ambayo imewahi kuwakilishwa na Ronaldinho.

VAN DIJK YAKARIBIA KUMPATA LIVERPOOL


Liverpool wanakaribia kushinda mbio za kumsajili beki wa kati wa Southampton Virgil van Dijk,  BBCimeripoti.

Makala hiyo inadai kuwa beki huyo wa Kidachi ameshaonesha ishara kwamba Anfield ndipo anapotamani kutua, Chelsea na Manchester City watakosa fursa ya kumsajili.

HART NDANI YA ORODHA YA MAN UTD

Manchester United wamemwinginza Joe Hart kwenye orodha ya makipa wanaohitaji kuwasajili ikiwa watamuuza David de Gea kwa Real Madrid, kwa mujibu wa  Daily Mail .

Jose Mourinho pia ataangalia uwezekano wa kumsajili Samir Handanovic wa Inter na Gianluigi Donnarumma wa Milan iwapo De Gea ataondoka Old Trafford.

REAL YATOA €135M KWA AJILI YA MBAPPE

Real Madrid wapo mbioni kutoa euro milioni 135 kumsajili mshambuliaji wa AS Monaco, Kylian Mbappe, kimedai  RMC Sport .

Habari hizo zinadai Los Blancos wapo tayari kumuuza James Rodriguez - Manchester United na Inter zikionekana kuvutiwa na biashara hiyo - na wanatumai kupata euro milioni 70 zitakazowasaidia kumpata Mbappe.

ARSENAL YAZUNGUMZA NA LACAZETTE

Arsenal wameonyesha nia ya kutaka kumsajili Alexandre Lacazette wa Lyon baada ya harakati zake kutimkia Atletico Madrid kugonga mwamba,  France Football imeripoti.

Mfaransa huyo amekiri timu kuwepo kwenye Ligi ya Mabingwa si kigezo, lakini Arsenal wanasemekana kuwa tayari kutoa euro milioni 40, ambazo ni 20 pungufu ya kiasi wanachokitaka miamba hao wa Ufaransa.

BARCA YAMLENGA DEMBELE

Barcelona wanajipanga kuanza upya mchakato wa kumsajili Osmane Dembele kutoka Borussia Dortmund kwa mujibu wa Mundo Deportivo .

Miamba hao wa Hispania walishindwa kuipata saini yake majira ya joto msimu uliopita, lakini sasa wanajiamini zaidi kuwa watafanikiwa.

LIVERPOOL YAPANGA KUZUNGUMZA NA LACAZETTE

Liverpool wanajipanga kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Alexandre Lacazette, kwa mujibu wa Daily Express .

Mipango ya Mfaransa huyo kwenda Atletico Madrid imevurugika, na Reds wanataka kuipiku Manchester United kuinasa saini yake.

EVERTON YAMUWINDA VARDY

Everton wanataka kumsajili mshambuliaji wa Leicester City Jamie Vardy, kwa mujibu wa  Sunday Express .

Toffees wanaweza kumpoteza Romelu Lukaku majira ya joto msimu huu, na wanaamini Vardy atakuwa mbadala wake sahihi.

LIVERPOOL YAKARIBIA KUMSAJILI SALAH

Liverpool wanakaribia kufanya usajili wa rekodi wa klabu kwa kumleta winga wa Roma Mohamed Salah Anfield, kwa mujibu wa Daily Telegraph .

Reds wapo tayari kulipa zaidi ya paundi milioni 35 kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri, mchakato unaweza kukamilika ndani ya wiki moja.

ARSENAL YAMPA WENGER BAJETI YA £150M

Arsenal wanatarajia kufanya usajili wa maana msimu wa majira ya joto baada ya kumpatia Arsene Wenger kitita cha paundi milioni 150 kwa ajili ya manunuzi ya wachezaji, limeripoti  Daily Star .

Mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe yumo kwenye rada za klabu hiyo ya London, kadhalika Riyad Mahrez wa Leicester.

MAN UTD YATAJA BEI YA DE GEA

Manchester United wapo tayari kumruhusu David De Gea kujiunga na Real Madrid majira ya joto, ila tu ikiwa miamba hao wa Hispania watakuwa tayari kutoa paundi milioni 80.

Real bado wanataka kumsajili, hata hivyo  Daily Mail  limeripoti kuwa United watamuuza kama ofa sahihi itawajia.

ARSENAL YAMPA MKATABA MPYA HOLDING

Beki wa kati wa Arsenal Rob Holding yupo mbioni kusaini mkataba mpya na klabu ya Arsenal kwa mujibu wa  The Mirror.

Mchezaji huyo aliyetua kutokea Bolton kwa dili la paundi milioni 2.1, ameonyesha uwezo mkubwa msimu wake wa kwanza Emirates na atapata thawabu ya bidii yake..

MAN UTD YAINGIA MBIO ZA MBAPPE

Manchester United ni klabu nyingine ya Ulaya ambayo ipo kwenye mbio za kumwania nyota wa Monaco, Kylian Mbape, kwa mujibu wa habari za  The Sun .

Real Madrid na Arsenal pia zimeonyesha nia ya kumsajili kinda huyo, lakini Man United wanaweza kuwa tayari kutoa dau nono la kuvunja rekodi ya Paul Pogba kumsajili Mfaransa huyo.

VALENCIA YAMTAKA HERRERA

Kiungo wa Manchester United Ander Herrera ameingia kwenye rada za Valencia ya Hispania, kwa mujibu wa  Sunday Mirror .

Mashetani Wekundu hawapo tayari kumuuza, lakini Valencia watatoa zaidi ya paundi milioni 30 kuishawishi United kumwachia.

KIBARUA CHA ZLATAN MAN UTD KIMEKWISHA

Zlatan Ibrahimovic amecheza mechi yake ya mwisho Manchester United kwa mujibu wa Daily Express .

Mkataba wa Mswidi huyo wa miezi 12 unafika mwisho Juni 30 na kufuatia majeraha yake ya Aprili, Mashetani Wekundu wamemtaarifu mchezaji huyo kuwa hatapewa mkataba mpya. 

MADRID WANATAKA KUMUUZA BALE MAN UTD

Real Madrid wapo tayari kuzungumza na Manchester United kuhusu uhamisho wa Gareth Bale, kwa mujibu wa The Independent .

Real wanataka kusajili mchezaji mwingine matata wa safu ya mashambulizi majira ya joto, Eden Hazard wa Chelsea na Kylian Mbappe wa Monaco wakiwa shabaha yao kuu na wanaweza kumuuza Bale ili kupata fedha za kufanyia usajili.

Hata hivyo mchezaji huyo hawezi kutoka kwa bei chee, ataigharimu United kiasi cha takribani paundi milioni 100.

BARCA YATETA NA SEMEDO KWA HERUFI KUBWA

Barcelona wapo katika mazungumzo yaliyochangamka na Nelsen Semedo wa Benfica, kwa mujibu wa  Record .

Semedo anaweza kupatakana kwa paundi milioni 69 kama bei iliyopangwa na klabu yake, lakini Barca wanakaribia kumnasa kwa paundi milioni 43.

MAN UTD YAANDAA DAU LA PERISIC

Manchester United wapo tayari kutoa dau la euro milioni 52 kwa ajili ya winga wa Inter Milan Ivan Perisic, Gazzetta dello Sport limeripoti.

United wanataka kuimarisha zaidi na kukifanya kipana kikosi chao na tayari wameshatenga dau la euro milioni 30 kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Croatia.

LIVERPOOL YAWANYATIA SALAH & BALDE

Liverpool bado wanaendelea na mazungumzo katika mchakato wao wa kuifukuzia saini ya Mohamed Salah kutoka Roma, pia wanavutiwa na Kieta Balde Diao kutoka Lazio, kwa mujibu wa ESPN .

CHELSEA WANAMTAKA ALVES

Chelsea, Manchester City na Tottenham wanafikiria kumsajili Dani Alves majira ya joto, kwa mujibu wa Daily Mail .

Mbrazili huyo anaaminika kuwa tayari kuondoka Juventus mwisho wa msimu huu, Conte akiwa shabiki wake mkubwa anataka kumleta Darajani ampe changamoto Victor Moses.

ARSENAL YAJIUNGA MBIO ZA MBAPPE

Arsenal nayo imeingia kwenye mbio za kuifukuzia saini ya nyota wa Monaco Kylian Mbappe, kwa mujibu wa  L'Equipe . 

Kinda huyo amezivutia klabu nyingi Ulaya, Real Madrid na Manchester United zikiwa klabu zenye nafasi kubwa zaidi kuinasa saini yake.

Lakini Arsene Wenger akiwa amesaini mkataba mpya tena, Gunners wapo tayari kutoa hadi euro milioni 100 kumleta nyota huyo kinda uwanja wa Emirates. 

No comments:

Post Bottom Ad

Pages