ERICK KYARUZI "MOPA" ATIMKA KAGERA SUGAR AELEKEA KLABU HII.. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Thursday, 22 June 2017

ERICK KYARUZI "MOPA" ATIMKA KAGERA SUGAR AELEKEA KLABU HII..Klabu ya Mbeya City maarufu kama Wagonga Nyundo wameanza kukiimarisha kikosi chao tayari kwa msimu ujao wa ligi kuu na kombe la FA baada ya kumsajili beki wa kati wa Kagera Sugar, Erick Kyaruzi Mopa. 

Kyaruzi amejiunga na Mbeya City kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu kwa dau ambalo halijawekwa wazi. 

Msimu uliopita Kyaruzi pamoja na kipa wake Hussein Sharif ‘Casillas’ walisimamishwa na uongozi wa Kagera Sugar kwa tuhuma za kuhujumu timu, walipocheza dhidi ya Young Africans na kufungwa mabao 6-2 nyumbani CCM Kaitaba. 

Kyaruzi anakuwa mchezaji wa kwanza kujiunga na Mbeya City tangu dirisha la usajili lilipofunguliwa Juni 15.

Down load app hii moja kwa moja kwenye kifaa chochote cha Android ili kupata habari kutoka vyankende.com 👉👉http://www.androidcreator.com/apk/app204631.apk

No comments:

Post Bottom Ad

Pages