DONALD NGOMA NA NIYONZIMA KUTUA SIMBA,HUKU WAFUATAO RUKSA KUONDOKA MSIMBAZI.. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Monday, 5 June 2017

DONALD NGOMA NA NIYONZIMA KUTUA SIMBA,HUKU WAFUATAO RUKSA KUONDOKA MSIMBAZI..Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema timu yake imechoshwa na kauli zisizoeleweka za wachezaji Jonas Mkude, Abdi Banda na Ibrahim Ajibu kuhusu usajili mpya, hivyo kamaa wanataka kuondoka ruksa, GLOBAL TV online iliripoti.

Mikataba ya wachezaji hao tayari imemalizika mwishoni mwa msimu uliopita na sasa wanatajwa kuondoka kwenda kwenye moja za klabu za hapa nchini.


Taarifa kutoka ndani ya Simba zimedai kuwa Donald Ngoma na Haruna Niyonzima wa Yanga wanakaribia kumwaga wino wa miaka miwili kutua Msimbazi, kwa mujibu wa Shaffihdauda .

Simba imekuwa ikiwawania Ngoma na Niyonzima tangu msimu uliopita ambapo sasa imeonekana kukaribia kuwanasa wote wawili kutokana na mikataba yao kufikia ukingoni. Ingawa italazimika kupunguza baadhi ya wachezaji wake wa kigeni kutimiza idadi ya wachezaji saba.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages