DEUS KASEKE NGOMA INOGILE.. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Friday, 2 June 2017

DEUS KASEKE NGOMA INOGILE..


WINGA wa Yanga, Deus Kaseke, amemaliza mkataba na timu hiyo lakini kuna taarifa kwamba mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara bado wanahitaji huduma ya mchezaji huyo waliyemsajili kutoka Mbeya City na yeye yupo tayari kusaini mkataba mpya, lakini endapo tu watampa ofa nono.

Kaseke anatajwa pia kuwaniwa na Simba lakini bado hajatoa maamuzi ya mwisho ya kusaini mkataba na washindi hao wa Kombe la FA ambapo ameomba apewe muda ili atafakari zaidi kuelekea msimu ujao.

Simba wana malengo na Kaseke na wamefanya naye mazungumzo ya awali huku Yanga nao wakifanya mazungumzo naye pia.

Meneja wa mchezaji huyo, William Milamo, aliliambia Mwanaspoti: “Mchezaji hakupata mapumziko kwa kipindi kirefu na ameomba kupumzika ndipo mambo mengine yaendelee, hivyo tumekubaliana baada ya wiki mbili ndipo ianze michakato mingine, ila ni mchezaji huru na popote anaweza kucheza kikubwa ni kufikia makubaliano.”     

No comments:

Post Bottom Ad

Pages