BEKI WA KLABU MOJA HUKO ALGENTINA AMCHOMA SINDANO MPINZANI WAKE. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Thursday, 15 June 2017

BEKI WA KLABU MOJA HUKO ALGENTINA AMCHOMA SINDANO MPINZANI WAKE.


Beki Federico Allende, wa klabu ya kiwango cha chini kwa michezo ya Pacifico , alijivuna kwenye mahojiano ya radio jinsi alivyotumia sindano kumdunga mara kadhaa mpizani wake wa klabu ya juu ya Estudiantes.
Allende amesema wachezaji walihitaji kuwa werevu ili kupata ushindi.
Rais wa shirikisho la soka la Pacifico Hector Moncada ameapa kumfukuza mchezaji huyo.
''Tumekasirishwa sana. Kisa hicho kimeharibu kazi nzuri ya timu . Nitamfukuza kutoka kwa klabu.'' Bw Moncada aliambia gazeti la Clarín.'
Pacifico ilishinda mechi hiyo kwa magoli 3-2 na kuibandua Estudiantes nje ya mashindano kwa uchungu mkubwa.
Wachezaji hao walikaribishwa nyumbani kama mashujaa katika mji mdogo wa magharibi wa Jenerali Alvear waliporudi kutoka Buenos Aires, pale mechi ilipochezwa.


No comments:

Post Bottom Ad

Pages