BAADA YA SERENGETI BOYS KUONDOSHWA MICHUANO YA KIMATAIFA KOCHA SHIME ATIMKIA HUKU.. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Tuesday, 6 June 2017

BAADA YA SERENGETI BOYS KUONDOSHWA MICHUANO YA KIMATAIFA KOCHA SHIME ATIMKIA HUKU..

a mkuu aliyekiongoza kikosi cha Serengeti Boys kwenye fainali za AFCON U17 2017 Bakari Shime ‘Mchawi mweusi’ amesema, licha ya kikosi cha JKT Ruvu kushuka daraja bado ataendelea kuwa nacho na atahakikisha anakirejesha ligi kuu Tanzania bara.

Shime amesikika akitoa msimamo wake Juni 5, 2017 kupitia Sports Extra ya Clouds FM alipozungumza na Said Karsandasi kutoka jijini Tanga.

“Maisha Yangu yapo kwenye kufundisha mpira, kila wakati napenda niishi nikifundisha, niliondoka nikiwa nafundisha JKT Ruvu na kwa bahati mbaya imeshuka daraja bado nitaendelea kuwa nao, kushuka kwao kwangu sio tatizo sana nitaendelea kuifundisha JKT Ruvu hadi pale TFF watakapokuwa wamenipa maelekezo mengine.”

“Nitarudi tuone kama tunaweza kupanda daraja, sioni tatizo kwa sababu hata makocha wakubwa duniani wameweza kufanya hivyo vitu wameshuka na timu na wamepanda nazo kwa hiyo ni sehemu ya kazi na majukumu kwa hiyo kwa sasa siwezi kuwakimbia JKT Ruvu labda itokee ofa ya timu nyingine au kitu kingine.”

“Nimeondoka akili yangu ikiwa JKT Ruvu na nimerudi hivyo lakini kwa upande wa pili nina program na TFF ambazo nazo baada ya fainali zile uongozi utaelekeza nini cha kufanya kwa hiyo kupitia maelekezo hayo nitakuwa na picha rasmi ya mwelekeo katika kazi yangu ya kufundisha.”

Baada ya Serengeti kufuzu michuano ya AFCON U17, Shime aliachana na JKT Ruvu aliyokuwa akiifundisha kabla kisha kujiunga na Serengeti kwa ajili ya maandalizi ya kambi kabla ya kwenda Gabon.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages