BAADA YA CHILE SASA NI UJERUMANI - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Friday, 30 June 2017

BAADA YA CHILE SASA NI UJERUMANI

Usipitwe na breaking news mbalimbaliza michezo pamoja na tetesi zote za usajili,like page yetu ya facebook 👉👉 HAPA

Siku moja baada ya timu ya taifa ya Ureno kuondolewa katika michuano ya Mabara kwa kufungwa kwa mikwaju ya penati 3-0 dhidi ya timu ya taifa ya Chile katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza, usiku wa June 29 Ujerumani waliingia uwanjani kucheza nusu fainali ya pili dhidi ya Mexico.


Mchezo kati ya Ujerumani dhidi ya Mexico ulikuwa ni mchezo ambao unasubiri mshindi ambaye atacheza na Chile katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mabara 2017 inayoendelea nchini Urusi, Ujerumani wamefanikiwa kuingia fainali ya kuifunga Mexico kwa magoli 4-1.Ushindi ambao unakuwa ni watatu mfululizo kwa Ujerumani kupata dhidi ya Mexico wakiwa mara zote wamecheza June 29, toka alipoifunga June 29 1998 katika michuano ya Kombe la Dunia na June 29 2005 katika mchezo wa Kombe la Mabara.


Magoli ya Ujerumani yalifungwa na Leon Goretzka aliyefunga magoli mawili dakika ya 6 na dakika ya 8, Timo Werner dakika ya 89 na Amin Younes dakika ya 90 wakati goli pekee la kufutia machozi kwa Mexico lilifungwa na Marco Fabian dakika ya 89. Download app hii moja kwa moja kwenye kifaa chochote cha Android ili kupata habari kutoka vyankende.com 👉👉HAPA

No comments:

Post Bottom Ad

Pages