AZAM YOUTH LEAGUE KUENDELEA WIKENDI HII.. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Friday, 16 June 2017

AZAM YOUTH LEAGUE KUENDELEA WIKENDI HII..


Ligi ya Azam kwa vijana chini ya umri wa miaka 13 (Azam Youth League U-13) inatarajia kuendelea tena kesho Jumamosi ndani ya Uwanja wa Azam Complex kuanzia saa 3.00 subuhi.

Wenyeji Azam Academy wanatarajia kufungua dimba kwa kuvaana na JMK Park, ikifuatiwa na vita nyingine kati ya Rendis FC na Ilala Academy, huku mchezo wa mwisho ukiwa kati ya Bom Bom SC na Magnet Youth.

Wakati zikielekea mechi hizo za raundi ya nne, matokeo ya wikiendi iliyopita ilishuhudiwa Azam Academy ikiichapa Magnet Youth mabao 2-1, Bom Bom ikiidungua Rendis bao 1-0 huku JMK Park ikiipa dozi kali ya 5-2 Ilala Academy.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages