Azam yapata mwaliko,kukipiga na timu hii kutoka Rwanda - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Thursday, 29 June 2017

Azam yapata mwaliko,kukipiga na timu hii kutoka Rwanda

Usipitwe na breaking news mbalimbaliza michezo pamoja na tetesi zote za usajili,like page yetu ya facebook 👉👉 HAPA


Klabu ya Soka ya Azam, jana jioni imeanza rasmi mazoezi ya kujiandaa na Mchezo wa Kirafiki dhidi ya Mabingwa wa ligi Kuu nchini Rwanda Rayon Sports utakaopigwa Julai 8 Mwaka huu Mjini Kigali.

Awali Azam FC ilipanga kuanza maandalizi ya msimu mpya Jumatatu ijayo Julai 3, lakini kutokana na mwaliko huo imeamua kuanza mazoezi mapema, ambapo Rayon imealika kwa ajili ya kucheza nao mchezo wa kirafiki ikiwa ni sehemu ya kusherehesha ubingwa walioutwaa.

Afisa Habari wa Klabu hiyo Jaffary Idd Maganga amesema mbali na hilo Lakini pia Rais wa Rwanda Paul Kagame Aliomba Azam walipeleke Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati CECAFA walilolitwaa mwaka 2015.

Aidha Maganga amesema kuwa Mara baada ya mchezo huo, uongozi umeamua kuwa utaendelea na Kambi ya kujiandaa na Ligi Kuu Soka Tanzania Bara Kwa msimu ujao.

-Ni Kama Pre Season hivyo baada ya kumaliza mchezo dhidi ya Rayon Sports tutaendelea na kambi huko huko Rwanda ikiwa ni Maandalizi ya msimu ujao pamoja na Mashindano mengine" Alisema Maganga.
 Download app hii moja kwa moja kwenye kifaa chochote cha Android ili kupata habari kutoka vyankende.com 👉👉HAPA

No comments:

Post Bottom Ad

Pages