ARSENAL YAZINDUA JEZI MPYA YATOA SUPRISE KWA MASHABIKI. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Thursday, 22 June 2017

ARSENAL YAZINDUA JEZI MPYA YATOA SUPRISE KWA MASHABIKI.


Klabu ya Arsenal imezindua jezi mpya ambazo zitatumika katika msimu mpya unaotarajiwa kuanza tarehe 12 ya mwezi wa nane mwaka huu.Katika uzinduzi huo Arsenal ilifanya kosa ambalo liliwafanya mamilioni ya mashabiki wa Arsenal kupagawa.
Kama ukitapa kununua jezi halisi za Arsenal huwa zinapatikana kwenye tovuti ya arsenaldirect.arsenal.com
ambapo kama unataka jezi yenye jina la mchezaji unayempenda unachagua jina la mchezaji huyo halafu inatokea jezi unalipa baadaye wanakutumia.
Lakini leo Arsenal ilifanya kosa ambapo ukichagua jina la Danny Welbeck ilikuwa ikitokea jezi namba saba mgongoni ambayo kwa kawaida huvaliwa na Alexis Sachez.
Arsenal yafanya kosa la mwaka-mashabiki wa Arsenal wapagawa
Hali hiyo iliamsha taharuki katika mitandao ya kijamii ambapo mashabiki wengi wa Arsenal waliichukulia kama ni ishara ya kwamba nyota huyo kutoka Chile ameshakamilisha mipango ya kuihama Arsenal.
Baada ya muda kidogo inaonekana lilikuwa ni kosa la kibinadamu tu kwani walifanikiwa kubadilisha na kwa sasa jezi ya Welbeck inaonesha jezi namba 23 na jezi ya Alexis Sanchez inaonesha jezi nampa 7.
Pia Alexis Sanchez alionekana katika video na picha za uzinduzi huo hizo ni dalili njema za kwamba Alexis Sanchez bado yupo sana tu.


Down load app hii moja kwa moja kwenye kifaa chochote cha Android ili kupata habari kutoka vyankende.com 👉👉http://www.androidcreator.com/apk/app204631.apk

No comments:

Post Bottom Ad

Pages