Arsenal kama Yanga Usajili msimu huu. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Wednesday, 28 June 2017

Arsenal kama Yanga Usajili msimu huu.

Usipitwe na breaking news mbalimbali za michezo pamoja na tetesi zote za usajili Tanzania na Ulaya,like page yetu ya facebook 👉👉 HAPA

Everton wanakaribia kumnunua mshambuliaji chipukizi wa Nigeria anayevuma sana Henry Onyekuru kutoka klabu ya KAS Eupen ya Ubelgiji.

Wanatarajwia kumnunua mchezaji huyo kwa £7m.

Onyekuru, 20, alifunga mabao 22 katika klabu hiyo inayocheza ligi kuu ya Ubelgiji msimu uliopita.

Alikuwa amehusishwa na kuhamia Arsenal, West Ham United na klabu nyingine kadha Ulaya zilikuwa pia zinamtaka.


Hata hivyo, mchezaji huyo, inaarifiwa tayari alifanyiwa uchunguzi wa kimatibabu Everton siku ya Jumatatu.

Onyekuru anatarajiwa kutumwa Anderlecht kwa mkopo mwaka mmoja, aendelee kuimarika akicheza soka Ubelgiji.

Anachukuliwa na mkurugenzi wa soka wa Everton Steve Walsh pamoja na meneja Ronald Koeman kuwa mchezaji atakayewafaa sana siku za usoni.

Onyekuru alichezea timu ya taifa ya Nigeria mara yake ya kwanza katika mechi ya kirafiki dhidi ya Togo mapema mwezi huu ambayo walishinda 3-0. Download app hii moja kwa moja kwenye kifaa chochote cha Android ili kupata habari kutoka vyankende.com 👉👉HAPA.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages