Ni kipindi cha mapumziko kwa wachezaji na makocha wa klabu zote baada ya msimu mrefu wa Ligi Kuu kufikia kikomo mwanzoni mwa mwezi wa Tano lakini nyota kadhaa wamekuwa wakitumia kipindi hiki kujiweka sawa kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2017/2018
Kupitia akaunti ya instagram ya mlinzi wa Yanga, Andrew Vincent maarufu kama "Dante" ameposti video ikimuonesha yuko ufukweni na mlinda mlango ambaye amemaliza mkataba wake na Yanga Deo Munishi "Dida", wakijiweka sawa kwa ajili ya msimu mpya
Ligi Kuu Bara inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi wa nane, kwa ajili ya msimu mpya wa 2017/2018