ALLY MAYAI AAHIDI KULIPELEKA SOKA LA TANZANIA MBELE. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Tuesday, 20 June 2017

ALLY MAYAI AAHIDI KULIPELEKA SOKA LA TANZANIA MBELE.


Kiungo wa zamani wa klabu ya Yanga na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars, Ally Mayayi leo amrudisha fomu za kuwania Urais wa Shirikisho la soka Tanzania TFF, baada ya kukamilisha taratibu ya kuzijaza.
Mayai ameiambia Goal , ameingia kwenye kinyang’anyiro hicho baada ya kujipima na kuona anaouwezo wa kuongoza soka la Tanzania baada ya kuwa na uzoefu na mchezo kwa muda mrefu.
“Nataka kuupeleka mbele mpira wa Tanzania najua njia na nyezo za kutumia ili Tanzania iweze kupiga hatua kuelekea kwenye mafanikio kama ilivyo mataifa mengine ya Afrika yalivyoendelea kwaiyo leo nimerudisha fomu na baada ya kampeni kuanza nitaongea mikakati yangu kwa wajumbe ili waweze kunipigia kura,”amesema Mayayi.
Kiungo huyo amesema mbali na dhamira aliyokuwa nayo katika kulipigania soka la Tanzania lakini pia wapo baadhi ya watu wanaomuona anaweza kazi hiyo wamemshawishi ili kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho ambacho anaamini kama haki itatendeka yeye ndiyo atakayekuwa mshindi.
Mayayi amesema anamuheshimu sana kiongozi anayemaliza muda wake Jamali Malinzi, lakini  ameingia kwenye zoezi hilo ili na yeye kutumia haki yake ya kidemokrasia kwa ajili ya kuusaidia kuuinua soka la Tanzania.
Amesema Malinzi amefanya mambo mengi mazuri, lakini anatakiwa kusaidiwa na watu wa kumsaidi ni yeye ambaye anauzoefu mkubwa na mchezo huo kutokana na kuucheza lakini pia kuusomea.
Mayayi ni mmoja wa watu waliojiingiza kwenye kuwania uongozi kwa nafasi ya Urais wengine waliojitokeza kwenye nafasi hiyo ni Rais anayemaliza muda wake Jamali Malinzi, Athuman Nyamlani, Shija Richard, Iman Madega,Wallece Karia  na Fredrick Msolwa.
Uchaguzi huo umepangwa kufanyika Agosti 12 mkoani Dodoma mwaka huu ambapo ndipo watapatikana viongozi wapya wa kuiongoza TFF, kwa miaka minne ijayo.


Down load app hii moja kwa moja kwenye kifaa chochote cha Android ili kupata habari kutoka vyankende.com 👉👉http://www.androidcreator.com/apk/app204631.apk

No comments:

Post Bottom Ad

Pages