AJIBU HUYOO JANGWANI MAMBO YAKO HIVI - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Thursday, 15 June 2017

AJIBU HUYOO JANGWANI MAMBO YAKO HIVI

Image result for ibrahim ajibu singida united
Habari kutoka ndani ya klabu ya Yanga zinasema kuwa mchezaji huyo amefikia pazuri kusaini Yanga ingawa tatizo lipo kwenye masuala ya fedha za usajili ambapo ameweka msimamo wa kutopokea pesa nusu kama walivyomuomba ili nusu wammalizie hapo baadaye.
Simba wao wanaonekana kutokuwa na haraka naye kwani tayari wamemsajili mshambuliaji mwingine John Bocco ambaye anadaiwa kuwa ataziba nafasi ya Ajibu. Hata hivyo vigogo hao wa Simba wamegawanyika kwani wapo wanaohitaji abaki na wengine wanataka aondoke.
“Jana (juzi) Ajibu alizungumza na watu wa kamati ya usajili na kungekuwepo na pesa taslimu basi wangempa na kumsainisha, Ajibu ameweka msimamo wa kulipwa pesa yake yote, hivyo kuna mvutano kidogo ambao tunaamini tunaweza kuushinda,” alisema kiongozi huyo.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages