WAFAHAMU HAPA WAAMUZI WA FAINALI YA FA KATI YA SIMBA NA MBAO - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Friday, 26 May 2017

WAFAHAMU HAPA WAAMUZI WA FAINALI YA FA KATI YA SIMBA NA MBAOKwa mujibu wa Kanuni ya 13 ya michuano ya Azam Sports Federation Cup HD msimu wa 2016/17, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemteua Ahmed Kikumbo wa Dodoma kuwa mwamuzi wa mchezo wa fainali kati ya Simba SC na Mbao SC utakaofanyika Uwanja wa Jamburi Mei 27, 2017 kuanzia saa 10.00 jioni.

Kikumbo atasaidiwa na Mohammed Mkono wa Tanga na Omary Juma wa Dodoma wakati mwamuzi wa akiba ni Florence Zablon pia wa Dodoma wakati Kamishna wa mchezo huo atakuwa Peter Temu wa Arusha. 

TFF inazitakia timu zote, Simba, Mbao, Waamuzi pamoja na Kamishna wao pamoja na wanafamilia wa mpira wa miguu, mchezo mzuri wenye fanaka kwa kila upande.

Alfred Lucas Mapunda

Ofisa Habari na Mawasiliano TFF

No comments:

Post Bottom Ad

Pages