TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO MAY 27. 2017... - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Saturday, 27 May 2017

TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO MAY 27. 2017...


UNITED INAWATAKA GRIEZMANN, LUKAKU & BELOTTI

Jose Mourinho yupo tayari kutumia fedha za kutosha kuiboresha safu yake ya mashambulizi Manchester United, kwa mujibu wa Daily Mail .

Mashetani Wekundu wanataka kumsajili Antoine Griezmann wa Atletico Madrid, Andrea Belotti wa Torino na Romelu Lukaku wa Everton kuziba pengo la Zlata Ibrahimovic na Wayne Rooney. Beki wa Burnley Michael Keane pia yumo kwenye rada.
MOURINHO ANAMTAMANI LUCAS

Jose Mourinho anatarajia kusajili winga wa kulia majira ya joto na amemgeukia Lucas Moura wa Paris Saint-Germain, kwa mujibu wa SportWitness .

Bosi huyo wa Manchester United atajaribu kwa mara nyingine kumsajili Mbrazili huyo baada ya kupata ugumu kuishawishi Chelsea kumuuza Willian.

INTER WANAWATAKA JAMES & PEPE


Inter wanataka kukamilisha usajili wa wachezaji wawili wa Real Madrid Pepe na James Rodriguez uhamisho wa majira ya joto, kwa mujibu wa Sportitalia .

Kadhalika Manchester United nao wametajwa kuifukuzia saini ya Mcolombia James ambaye anataka kuondoka Madrid majira ya joto baada ya kushindwa kumshawishi Zinedine Zidane.

MOU ANAMTAKA MORATA KAMA SEHEMU YA BIASHARA YA DE GEA


Manchester United wanataka Alvaro Morata awe sehemu ya biashara iwapo Real Madrid itamsajili kipa wao David de Gea katika uhamisho wa majira ya joto,  Marca  limeripoti.

AC Milan nayo imeibukia kuifukuzia saini ya Morata, lakini United watakuwa tayari kupunguza bei ya De Gea kutoka euro milioni 75 hadi 25 ikiwa Morata atahama kutoka Real Madrid kutua Old Trafford. 

MADRID YALENGA KUMSAJILI BONUCCI


Real Madrid imepania kumsajili beki wa Juventus Leonardo Bonucci usajili wa majira ya joto kwa mujibu wa gazeti la Hispania  Don Balon .

Los Blancos wanataka kuimarisha safu yao ya ulinzi kwa ajili ya msimu ujao kwani muda wowote Pepe anaweza kuondoka Bernabeu.

ARSENAL YAMPA DAU NONO ALEXIS


Arsenal wamempa Alexis Sanchez mkataba mpya wenye thamani ya paundi 270,000 kwa wiki baada ya Bayern Munich kuonyesha nia ya kumsajili, kwa mujibu wa  Daily Mail .

Mkataba huo bado unapungua zaidi ya paundi 300,000 anazotaka Alexis Sanchez lakini atapata marupurupu.

AUBAMEYANG AOMBA KUONDOKA


Pierre-Emerick Aubameyang ameomba kuondoka Borussia Dortmund, kwa mujibu wa  Bild .

Ingawa Paris Saint-Germain, AC Milan na Tianjin Quanjian zinataka kumsajili mshambuliaji huyo, bado hajafanya uamuzi ni klabu gani atajiunga nayo.

Klabu hiyo ya Ujerumani tayari imeshachagua mchezaji wa kuziba pengo lake Patrik Schichk wa Sampdoria.

ROONEY KUTIMKIA CHINA


Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney anatarajia kutimkia China majira ya joto kwa mujibu wa Daily Mirror .

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza amekuwa akihusishwa mara kwa mara na klabu za Mashariki ya Mbali na inaaminika ameshaamua kuondoka Ligi Kuu Uingereza majira ya joto.

MONACO YAMFUKUZIA BATSHUAYI


Monaco imeungana na West Ham katika mbio za kumfukuzia mshambulizi mahiri wa Chelsea Michy Batshuayi, kwa mujibu wa Sun .

Mbelgiji huyo alifunga goli ambalo liliishindia Blues taji dhidi ya West Brom lakini anaweza kuondoka Darajani Stamford baada ya kukosa nafasi chini ya Antonio Conte.

NEWCASTLE YATOA DAU LA £39M KWA AJILI YA CARVALHO


Newcastle United wameandaa dau la paundi milioni 39 kwa ajili ya kiungo wa Sporting, William Carvalho, kwa mujibu wa chanzo cha Ureno O Jogo na  Record .

BARCA YAMFUKUZIA HERRERA


Barcelona wanajipanga kumsajili kiungo wa Manchester United Ander Herrera, kwa mujibu wa  Sport .

Bosi mpya ajaye Barca Ernesto Valverde alifanya kazi na Herrera Athletic Bilbao na anataka kufanya kazi tena na mchezaji huyo.

Herrera ambebakiwa na mwaka mmoja tu kwenye mkataba wake Old Trafford na Blaugrana wanaamini watafanikiwa kumshawishi kutosaini mkataba mpya.

ARSENAL YAMTOLEA MACHO HAZARD


Arsenal wanataka kumsajili winga wa Borussia Monchengladbach Thorgan Hazard, kwa mujibu wa  Jeunes Footeux .

Mchezaji wa kimataifa wa Ubelgiji, ambaye ni kaka wa Eden wa Chelsea, na Arsene Wenger amevutiwa na kiwango chake thamani yake ikiwa ni euro milioni 18.

JUVENTUS YAMFUKUZIA RENATO SANCHES


Juventus wapo tayari kuipiku Manchester United katika mbio za kumwania Renato Sanches kutoka Bayern Munich kwa mujibu wa The Sun .

Kiungo huyo kinda ameanza mechi sita tu msimu huu na United wapo tayari kutoa ofa kwa ajili ya mchezaji huyo waliyemkosa majira ya joto msimu uliopita.

Usikose kuunga nasi kila siku kupata habari mbalimbali za kikimchezi pia unaweza kutmbea nasi kiganjani mwako kwa kupakua app yetu bonyeza HAPA kudownload

No comments:

Post Bottom Ad

Pages