TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA JUMATATU YA MAY 29/05/2017. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Tuesday, 30 May 2017

TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA JUMATATU YA MAY 29/05/2017.


BAADA ya kutwaa taji la FA kwa ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Chelsea, Hatimaye kocha wa Arsenal, Arsene Wenger atasaini mkataba wa miaka miwili wa kuifundisha klabu hiyo ya Emirates. (#The_Times)·

KOCHA Jose Mourinho amewaambia Real Madrid kuwa atawapa David De Gea endapo na wao watamtoa Raphael Varane. (#Diarigol)·

WEST HAM inataka kumtumia nyota wake mpya waliyemsajili kutoka Manchester City, Pablo Zabaleta kumshawishi Mshambuliaji wa City, Kelechi Iheanacho ajiunge na West Ham. Staa huyo wa Nigeria ana thamani ya pauni £20m. (#The_Mirror)·

MANCHESTER CITY inataka kuweka rekodi ya Dunia ya kutaka kumsajili Mshambuliaji wa Monaco, Kylian Mbappe kwa dauni la pauni £114m. (#Telefoot)·

MANCHESTER UNITED haitamnunua Winga wa Inter Milan, Ivan Perisic baada ya kupungukiwa milioni £15. United imetoa £42m lakin i Inter wanataka pauni £55m kwa nyota huyo ambaye mwakani atatimiza miaka 30. (#Calciomercato)·

KOCHA wa Newcastle Rafa Benitez anataka kumrudisha England kipa wa Napoli, Pepe Reina. Wawili hao walifanya kazi pamoja klabuni Liverpool. (#The_Sun)·

OLYMPIQUE LYON imetoa pauni £12m ikitaka kumsajili Mshambuliaji wa Bayer Leverkusen, Javier Hernandez "Chicharito". (#RMC)·

STOKE CITY inataka kumsajili Mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney. (#Mirror)·

SWANSEA & BRIGHTON zimeingia kwenye vita kali ya kumtaka Mshambuliaji wa KAS EUPEN ya Ubelgiji, Henry Onyekuru. (#Daily_Mail)·

KIPA wa Chelsea Thibaut Courtois anatarajia kusaini mkataba mpya Stamford Bridge. (#Sky_Sports)·

MANCHESTER CITY inakaribia kumsajili Kipa wa Benfica, Ederson ili kuwapa changamoto makipa wake. (#Mirror)·

AC MILAN imeungana na klabu za Chelsea, Tottenham ikitaka kumsajili Mshambuliaji wa Celtic, Moussa Dembele. (#Express)·

ARSENAL inaonekana ipo mbioni katika harakati za kutaka kumsajili Mshambuliaji wa Torino, Andrea Belotti ambaye anatakiwa na klabu za Chelsea na Manchester United. (#Sun)·

KOCHA Jose Mourinho ameiambia bodi ya klabu hiyo kuwa wahakikishe Beki wa Burnley, Michael Keane anatua Old Trafford. (#Daily_Mail)·

WINGA MSHAMBULIAJI wa Monaco Thomas Lemar anawaniwa na vilabu vya Juventus, Atletico Madrid na Tottenham. (#L_Equipe)·

LEICESTER CITY inataka kumsajili Beki wa zamani wa Barcelona na Juventus, Martin Caceres ambaye ameachana na klabu ya Southamton hivi karibuni. (#Leicester_Mercury)·

BEKI wa Hull City, Harry Maguire huenda akajiunga na Tottenham au Everton kwa dau la pauni £22m. (#Mirror)·

INTER MILAN imeweka pauni £42m ikitaka kumsajili Kiungo wa Real Madrid, James Rodriguez. (#AS)·

MSHAMBULIAJI wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic amegoma kwenda China akidai kuwa hajamaliza kazi Old Trafford. (#Daily_Maily)·

CHELSEA  & MANCHESTER UNITED zipo kwenye mchuano mkali wa kuiwania saini ya Mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku. (#Express)·

WEST HAM inataka kumsajili Kiungo wa Everton, Ross Barkley.Staa huyo amegoma kusaini mkataba mpya Goodison Park.  (#Daily_Star)·

MANCHESTER UNITED imeweka pauni £25m kwa beki wa Benfica, Victor Linderlof. (#Mirror)·

No comments:

Post Bottom Ad

Pages